Friday, October 14, 2016

Saudia yaomba mkopo baada ya kukumbwa na hali mbaya ya kiuchumi

Hali ya kiuchumi nchini Saudia imezidi kuwa mbaya kiasi kwamba nchi hiyo imelazimika kuomba mkopo kutoka kwa mashirika ya kimataifa ya fedha.

Mtandao wa Intaneti wa The Wall Street Journal wa nchini Marekani uliandika katika toleo lake la tarehe 10 mwezi huu wa Oktoba kwamba, ufalme wa Saudia umekuwa ukitegemea sana pato lake kutokana na uuzaji mafuta ghafi nje ya nchi, lakini bei ya bidhaa hiyo muhimu imeporomoka tangu katikati ya mwaka 2014 na kuifanya Saudia ivunje rekodi katika nakisi ya bajeti yake, kwa kukumbwa na nakisi ya dola bilioni 98 za Kimarekani kwenye bajeti yake ya mwaka jana. 

Pia liliandika: Mwaka jana Saudia ilipata mkopo wa dola bilioni 10 kutoka kwa mashirika ya fedha ya kimataifa.  

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, kutokana na vita vya Yemen na uungaji mkono wake kwa magenge ya kigaidi kuigharimu fedha nyingi serikali ya Saudia sambamba na kuporomoka bei ya mafuta katika soko la dunia, nchi hiyo ya kifalme imelazimika kuomba mikopo katika mashirika ya kimataifa ya fedha ili kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi ilioikumba.

Duru nyingine za habari likiwemo shirika la habari la IRNA nazo zimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, utawala wa Aal Saud umeamua kuomba mkopo kutoka kwa Benki za HSBC na Citigroup za Marekani na kuchapisha dhamana za madeni (Eurobond).
Mohammad bin Salman Aal Saud, Waziri kijana wa Ulinzi wa Saudia ambaye uvamizi wake nchini Yemen umeisababishia Saudi Arabia hasara kubwa ya kifedha

Kwa upande wake, Benki Kuu ya Saudia imetoa mkopo wa dola bilioni nne wa masharti machache kwa benki za ndani ya Saudia ili kuzuia kufilisika baadhi ya mashirika makubwa nchini humo.

Takwimu zinaonesha kuwa, dhamana za madeni za Saudia kwa ajili ya kukabiliana na matatiso ya kiuchumi ya nchi hiyo zinaweza kupindukia dola bilioni 15 kiwango ambacho hakijawahi kufanyika nchini humo katika historia ya miongo kadhaa ya nchi hiyo.

Nakisi ya bajeti, mgogoro wa matumizi ya fedha taslimu, kuporomoka soko la hisa na kiujumla matatizo ya kifedha katika mfumo wa kibenki wa Saudia katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, yote ni mambo yaliyoathiriwa na njama za utawala wa Saudia za kupunguza thamani ya mafuta katika soko la dunia. 

Saudia ilifanya njama hizo kutoa pigo kwa baadhi ya nchi wapinzani wake kama vile Iran na Russia, lakini madhara ya njama hizo zimeirejea mwenyewe hivi sasa.

Misri yaitolea uvivu Saudia, yasema inaunga mkono magaidi Syria na Yemen

Gazeti la al-Watan la nchini Misri limeandika kuwa, utawala wa Aal-Saud ndio mdhamini mkubwa wa fedha na silaha kwa makundi ya kigaidi na Kiwahabi yanayofanya jinai na mauaji makubwa katika nchi za Syria na Yemen. 

Alkhamis ya jana gazeti hilo liliandika ripoti hiyo kwa mara ya kwanza dhidi ya Saudi Arabia na kubainisha kwamba, utawala wa Saudi Arabia ndio muungaji mkono mkubwa kwa magenge ya kigaidi.
Genge la kitakfiri na Kiwahabi la Jab'hatu Nusra
Sambamba na kushadidi mgogoro katika uhusiano wa Misri na Saudia kuhusiana na kadhia ya Syria, gazeti hilo la al-Watan limeandika kuwa, kwa muda wote Saudia imekuwa ikiyasaidia kijeshi na kifedha kwa makundi ya kigaidi likiwemo kundi la kigaidi na kitakfiri la Jab'hatu Nusra na mengine mengi ya Kiwahabi huko Syria na Yemen. Kwa mujibu wa gazeti hilo, Uturuki ni mhusika mkuu katika kuwasilisha misaada hiyo kutoka Saudia kwa makundi hayo nchini Syria.
Viongozi wa Uturuki na Saudia wanaotoa himaya kamiali kwa makundi potofu ya Kiwahabi
Limeenda mbali zaidi na kuandika kuwa, nchini Yemen baada ya Saudia kuunda muungano wa kijeshi ilioupa jina la 'Kimbunga' iliunda pia makundi ya kigaidi na kuyapa silaha na fedha kwa lengo la kupambana na harakati ya wananchi ya Answarullah.
Mgogoro kati ya Misri na Saudia ulishtadi baada ya Misri kuupigia kura ya ndio muswada wa Russia kuhusiana na kadhia ya Syria mbele ya Umoja wa Mataifa.

SHEIKH ALHAD MUSSA: WATANZANIA FATENI MAFUNDISHO NA MATENDO YA IMAN HUSSEIN (A.S) KWA KUTENDA HAKI NA KUKATAA DHULUMA

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum wa pili kutoka Kushoto akiwa katika matembezi ya Amani yaliyofanyika Jijini Dar es salaam yaliyoandaliwa na waumini wa Khoja Shia Ithanasheriya Tanzania ikiwa ni Ishara ya kumkumbuka Mjukuu wa mtume Muhamad ambaye ni Imam Hussein.

Akizungumza na wanahabari wakati wa maandamano hayo ya amani Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amewataka watanzania kufwata Nyayo za Iman Hussein ambaye alipenda haki na kukataaa dhuluma miongoni mwa Jamii pamoja na kutunza amani ilipo nchini Mwetu.

Aidha amezitaka Taasisi za kidini nchini kujenga Umoja na mshikamano miongoni mwao bila kujali imani na itikadi za dini zao ili kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano na upendo kwa wote.
 
 Waumini wa Dini ya kiislam Kutoka jumuiya ya kiislam Khoja Shia Ithnasheriya Tanzania wakiwa katika maandamano ya amani Jijini Dar es salaam  ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w),ambaye ni Imam Hussein (a.s),maandamano ambayo yameanzia katika msikiti wa Kablastan hadi msikiti wa Khoja Shia Ithnasheriya jijini dar es salaam
 
 Kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akizungumza na wanahabari wakati wa maandamano hayo Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine Sheikh Jalala amendelea kusisitiza watanzania kutunza  amani na umoja uliopo pamoja na kufwata yale ambayo Imam Hussein alikuwa akiyatenda wakati uhai wake ikiwemo kupinga ukandamizaji, dhuluma katika jamii na kujenga umoja na mshikamano katika jamii.