Monday, November 20, 2017

Tumetoka kwa Matembezi ya Amani ili kuoyesha Huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)-Sheikh Jalala


Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania Sheikh Hemed Jalala (wapili kushoto) na Sheikh Mkuu wa Jimbo la Dar es salaam la Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania (T.I.C) Sheikh Suleiman Serehani (wakwanza kulia) wakiongoza Matembezi ya Amani ya kukumbuka na kuomboleza Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), jana Jijini Dar es salaam.
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema Sababu kubwa inayowafanya Waislamu, hususani Waislamu Shia Ithnasheria Kutoka na kufanya Matembezi ya Amani  kuadhimisha kifo cha mtume ni kuionyesha jamii huruma ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwani Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa na huruma kwa watu wote.

“Miaka zaidi ya 1400 leo bado tunakumbuka Kifo cha Mtume Muhammd (s.a.w.w), kwanini tutoke katika matembezi haya ya amani tunayoyaonyesha katika ardhi yetu ya Tanzania, kwasababu Mtume Muhammad (s.a.w.w) alitumwa kuwa na huruma kwa watu wote” Alisema Sheikh Jalala.
 
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheria Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari, jana katika Matembezi ya Amani ya kukumbuka na kuomboleza Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), matembezi yaliyoanzia Ilala Boma hadi Viwanja vya Kigogo Jijini Dar es salaam.
Sheikh Jalala alisema hayo mwiho wa wiki wakati wa matembezi ya Amani ya kukumbuka na kuomboleza Kifo cha Mtume Mbora na mtukufu kwa watu wote ambae ni Muhammad (s.a.w.w), katika matembezi yaliyoanzia Ilala Boma hadi Viwanja vya Pipo Kigogo Dar es salaam.

“Siku ya Kuomboleza Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni siku ya kukumbuka Utu, Busara,Uwanadamu, kuwaheshimu wasiokuwa na Dini,kukaa vizuri pamoja na Wakristo, Mayahudi, wanaoabudu Masanamu na Mapagani  aliokuwa akiujali katika maisha yake” aliongeza Sheikh Jalala.
 
Sheikh Mkuu wa Jimbo la Dar e salaam la Waoslamu Shia Ithnasheria Tanzania (T.I.C) Sheikh Suleiman Serehani akiongea na Waandishi wa Habari katika Matembezi ya Amani yaliyofanyika jana kuanzia Ilal Boma hadi Viwanja vya Pipo Kigogo Jijini Dar e salaam
Aidha Sheikh Jalala alisema Mtume Muhammd (s.a.w.w) aliuwezi Waislamu kwa waislamu, Umoja wa Watu wote na alitengeneza Umoja kati yake na Wakristo, Mapagani na Mayahud , umoja huu ulikkuwa ni wa kumsaidia mtu yoyote ambae atashambuliwa hatimae akatengeneza Mazingira asiekuwa Mwislamu akishambuliwa Waislamu watanyanyuka kumsaidia na Waislamu wakishambuliwa watu wa Dini nyingine na Madhehebu nyingine watanyanyuka  kuwasaidia Waislamu.

“Napenda kuwaelekeza Viongozi wa Kidini Masheikh, Maustadhi, Makasisi, Maskofu, na Mashemas  kwamba Mimbari au Madhabahu yao Siku za Ijumaa au Siku za Jumamosi na Jumapili, Madarasa zao, Vyuo vyao vitumike katika kuleta na kuboresha Amani ya watanzania wote, katika kuleta maelewano, Mshikamano ya watanzania wote na Tiafa hili liendelee kuwa kisiwa cha Amani” Alisisitiza Sheikh Jalala

Mtume Muhammad (s.a.w.w) alifariki Dunia tarehe 28, Mwezi wa Safar, Mwaka 11 Hijiria kwa Mujibu wa Kalenda ya Kiislamu, Mtume alikufa akiwa na Umri wa miaka 63.

No comments: