Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amewataka
Watanzania Waislamu na Wasiokuwa Waislamu kusimamia na kutetea haki za Binadamu
yoyote na kupina aina yoyote ya Ugaidi kwani kufanya hivyo ndio moja ya mafunzo yanayopatikaka katika kuadhimisha
40 ya Imam Hussein (a.s), Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
“Tukio la 40
ya Imam Hussein (a.s) katika funzo la kwanza linabeba darasa la Ubinadamu,
Mwanadamu anahadhi, anaheshima, ni mtakatifu,nilazima aenziwe,ndio Uislamu
umekataza kumdhuru, kumnyanganya na ni haramu kumwaga Damu ya mwanadamu yoyote,
Mwanadamu awe Mwislamu, awe Mkristo, awe Pagani” Alisema Sheikh Jalala
Sheikh
Jalala alisema hayo wiki ilipita wakati akizungumza na waandishi wa Habari,
Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam na kusema kuwa 40 ya Imam Hussein inatoa
funzo la kupinga aina yoyote ya Ubaguzi,uwe ubaguzi wa Rangi,uwe ubaguzi wa
kidini,uwe ni ubaguzi wa Kifikra, ndio maana ukiangalia katika msafara wake wa
kiulekea katika Mji wa Karba nchini Iraq utakuta mtu anaeitwa John ambae ni
Mkristo.
Aidha Sheikh
Jalala amewataka Watanzania kutowanyanyapaa na kuwatenga watu ima katika
Umasikini wao, ima kwa ufakiri wao, ima kwa magonjwa yao, ima kwa mapungufu yao
walioumbwa nayo, walemavu wa ngozi, macho, masikio, miguu, mikono, na waadhirika
wa Madawa ya kulenya.
“Tukitaka
tufaidike na Rasilimali alizotupa Mungu ni lazima tuwe Wazalendo, Watanzania
tutakaposifika na Uzalendo, tutafaidika na Gesi yetu, ardhi yetu,Madini yetu,
mafuta yetu, Tanzania itajulikana kwamba ni Moja katika nchi inayotoa misaada
kwa nchi zingine, hii ni funzo tunayopata katika 40 ya Imam Hussein (a.s)”
Alisema Sheikh Jalala
Hata hivyo
Sheikh Jalala amesema kuwa unapowaona Waislamu wananyanyuka huku wakisema
Labayka ya Hussein (a.s) maana yake wanamuambia Hussein (a.s) wewe ulitoka
kupambana na aina yoyote ya Ugaidi, sisi tupo tayari kupambana na
kuusambaratisha aina yoyote ya Ugaidi, Ugaidi wa Kifikra, Kimtazamo, pia
waislamu na Wakristo tunahakikisha mafunzo tunayowafundisha watoto wetu
hayabebi fikra yoyote ta Ugaidi.
Imam Hussein
(a.s) ni Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), yeye ni Imam Hussein Ibn Ali (a.s)
Baba yake ni Imam Ali Ibn Abutwalib (a.s), Mama yake ni Fatuma Bint Muhammad
(a.s), Kaka yake ni Imam Hassan Ibn Ali (a.s), Dada yake ni Zaynab Bint Ali
(a.s), 40 ya Imam Hussein (a.s) ni siku ya arobaini baada ya kuuliwa yeye Imam
Hussein (a.s) na Maswahaba zake katika ardhi ya Karbala, nchini Iraq, mwaka wa
61 H.