Friday, May 5, 2023

HAKUNA HAKI BILA UWAJIBIKAJI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waajiriwa wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kufungua mafuzo elekezi kwa watumishi hao yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Wa pili kulia Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, James Kibamba wa Ofisi hiyo.

Watumishi wapya kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu Mkuu wa Serikali wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kuwa hakuna haki bila uwajibikaji katika Utumishi wa Umma.

Hayo yamesemwa leo tarehe 4 Mei, 2023 na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Sarah Mwaipopo wakati akifungua mafunzo elekezi kwa watumishi wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

Akizungumzia aina ya mafunzo yatakayotolewa, Bi. Mwaipopo amesema kuwa Ofisi hiyo imekusudia kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala mbalimbali yanayohusu majukumu yao, haki na wajibu wao kama watumishi wa umma, Muundo wa Serikali, taratibu za utendaji kazi, maadili, nidhamu, uadilifu na ustahimilivu ambavyo vyote kwa pamoja vinapaswa kuzingatiwa ili kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi wa umma hususan kwa ajira mpya.

Ameleza kuwa mafunzo hayo ni utekelezaji wa matakwa ya kisheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ambpo Ofisi imeona umuhimu wa kutenga bajeti ili kufanikisha mafunzo haya muhimu yatakayowajenga na kuwapa uelewa katika masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo, Bi. Mwaipopo amewaleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika kuimarisha utendaji kazi, nidhamu na maadili ikiwa ni pamoja kuwawezesha kuepuka makosa mbalimbali ya kinidhamu na yale ya kiutumishi ambayo yangeweza kufanyika kwa kukosa uelewa ili kuweza kuyaepuka wakiwa mahali pa kazi.

Aidha, amewataka watumishi wapya kujifunza na kuelewa vyema dira, dhima na misingi muhimu ambayo Taasisi imejiwekea katika utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya usimamizi wa mashauri ya madai na usuluhishi yanayofunguliwa na au dhidi ya Serikali, ndani na nje ya nchi.

Misingi hiyo inahusu uwajibikaji, uadilifu, uaminifu na weledi ambayo ikitekelezwa vyema ni nguzo ya maendeleo endelevu ya nchi yetu.

Naye Francis Oswald, Wakili wa Serikali ameishukuru Ofisi kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu ambayo yatawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamewahusisha watumishi 64 waajiriwa wapya wa Ofisi hiyo wa kada mbali mbali ikiwemo Mawakili wa Serikali 41, Maafisa TEHAMA 2, Makatibu sheria 4, Katibu Muhtasi 3, madereva 9, Watunza Kumbukumbu 4 na Afisa Usafirishaji mmoja.

VIONGOZI WA UMMA WASISITIZWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO

MKUU  wa Wilaya ya Mbeya Mjini  Mhe. Benno Malisa,amewataka Viongozi  wa  Umma  kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza katika kutekelezaji majukumu yao ya kila siku. 

Hayo ameyasema wakati  akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma wa Halmashauri mbili za Mkoa wa Mbeya ambazo ni halmashauri ya Jiji la Mbeya  na halmashauri ya Mbeya DC  yaliyoandaliwa na Sekretariti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yalifanyika katika Ukumbi wa Jengo la NHIF Jijini Mbeya.

o Mhe. Malisa alieleza kuwa ni dhahiri kuwa Viongozi wote katika Halmashauri hizo wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana kwa pamoja , kuwa na mawazo na uelekeo mmoja ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli zote za serikali na kuweza kuleta matokeo chanya kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Mhe. Malisa alifafanua kuwa serikali inapeleka fedha  nyingi  sana katika halmashauri mbalimbali  nchini kwa sababu ndipo kunakotekelezwa miradi mingi inayowagusa wananchi moja kwa moja kama vile maji, elimu , afya na nyingine nyingi

“Ndugu zangu  fursa hii tukaitumie vizuri ili matokeo ya fedha hizi yakaonekane wazi huu sio muda wa  kulumbana, sio muda wa kususiana majukumu,sio muda wa kunyoosheana vidole bali ni muda wa kuunda timu moja  , ni muda wa kila mmoja kuwajibika ipasavyo katika nafasi aliyo nayo na  kufanya kazi kwa bidii ili tukaaminike kwa viongozi wetu wa juu  ” alisema.

Aidha Mhe. Malisa aliendelea kusema kuwa  Viongozi wanapowajibika kwa pamoja itarahisha utendaji kazi wao wa kila siku wa kuhakikisha kuwa wananchi wanatekelezewa miradi yote kama ilivyopangwa jambo linakalowafanya wananchi  kuwa na Imani na viongozi wao na kuiamini serikali kwa ujumla wake “Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu” alisema.

Pamoja na hayo Mhe. Malisa alizungumzia suala  la mgongano wa maslahi kuwa limekua ni tatizo kubwa sana katika Halmashauri nyingi nchini. Suala hili limekua na changamoto nyingi katika kutekeleza miradi mbalimbali, Kiongozi anapokua na maslah binafsi katika mradi  fulani husababisha kucheleweshwa kwa miradi hiyo ama kutekelezwa kwa kiwango kisichoridhisha ama kutokutekeleza kabisa kutokana na mvutano unaokuepo  baina ya watekelezaji kwa sababu ya maslah binafsi.” Viongozi wenzangu hatukuteuliwa tukafanye kazi kwa kuangalia maslah yetu binafsi, tumeteuliwa tukawatumikie wananchi bila kutanguliza maslah yetu mbele tukatangulize maslah ya wananchi na Taifa kwa ujumla: alisema.

Awali akielezea dhumuni kubwa la   mafunzo hayo Katibu Msaidizi Kanda  ya  Nyanda za Juu kusini -Mbeya Bw, Pauline  Kanoni alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ina jukumu kubwa la kutoa elimu ya maadili kwa Viongozi wa Umma nchini ili kuwa na Viongozi waadilifu na wenye kuaminika kwa wanachi wao.

Pamoja na hayo Bw. Kanoni alisema kuwa mafunzo hayo yana lengo la kuwakumbusha Viongozi kuhusu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba  13  ya mwaka 1995. Katika kuzingatia sheria hii yapo mambo ambayo viongozi  wanapaswa kuzingatia wanapotekeleza majukumu yao  kwa kuzingatia kanuni za Maadili pamoja na misingi ambayo imewekwa kulingana na sheria na katiba , kuwa wawazi kwenye shughuli wanazofanya na kutumia rasilimali za Umma vizuri.

” Niwaase Viongozi kuwa na uwajibikaji wa pamoja katika kutekeleza majukumu yenu kwani haiwezekani Kiongozi anakwenda kinyume na maelekezo ya serikali , unakuta kingozi huyu anasema hivi mwingine anasema hivi hayo sio maadili viongozi wote wanapaswa kuwa na kauli moja“ alisema.

“Tunajua viongozi wetu sio kwamba hamna Maadili tunajua kuwa ni waadilifu wa kutosha lakini tumekuja kukumbushana tuu kwa sababu tunajua binadamu tunasahau hivyo tunakumbushana nini tunapaswa kufanya nini hatupaswi kufanya wakati wa utekelezaji wa majukumu yetu kwani kiongozi akikiuka maadili anaitia doa serikali yetu” alisema 

Naye mshiriki wa mafunzo hayo  Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bi. Amina Nalicho alisema kuwa ili kuweza kupata matokeo chanya kwa  serikali na wanachi  ni dhahiri kuwa Viongozi wanapaswa kufanya kazi kwa pamoja   “ kuna msemo usemao kidole kimoja hakivunji chawa” alisema. 

Katika mafunzo hayo ya siku moja yalitolewa  kwa viongozi wapya ambao ni wakuu wa idara na vitengo kutoka Halmashauri ya  Mbeya Jiji pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya . Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na Mada ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tamko la Rasilimali na madeni, mada ya Ahadi ya Uadilifu,Mada ya Mgongano wa maslah Pamoja na mada ya uwajibikaji wa Pamoja.