Saturday, April 25, 2015

UN: Saudia imeua maelfu ya watu nchini Yemen



Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba maelfu ya wananchi wa Yemen wameuawa katika mshambulizi yanayoendelea kufanywa na Suadi Arabia dhidi ya nchi hiyo.
Maiti za Watoto wa Nchini Yemen waliouwawa na Saudia Arabic.

Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Johannes Van Der Klaauw, amesema kuwa mashambulizi ya Saudia huko Yemen yameathiri maeneo yote ya nchi hiyo. 

Van Der Klaauw amesema kuwa, Umoja wa Mataifa unataka kupeleka vikosi vyake nchini Yemen haraka iwezekanavyo. 

Ameongeza kuwa kabla ya mashambulizi ya siku chache za hivi karibuni ya Saudia huko Yemen raia zaidi ya laki tatu walikuwa wamekimbi makazi yao na ametahadharisha kuhusu mgogoro mkubwa wa kibinadamu nchini humo.

Shirika la Afya Dunia (WHO) pia limetangaza kuwa tangu tarehe 19 Machi hadi 20 Aprili raia wasiopungua 1080 wakiwemo wanawake na watoto wadogo wa Yemen wameua katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Saudia dhidi ya nchi hiyo.

Saudia yaogopa kivuli chake, ina woga itashambuliwa

Duru za usalama nchini Saudi Arabia zimetangaza hali ya tahadhari kufuatia ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo juu ya kuwepo uwezekano wa kushambuliwa vikali na upande ambao haikuutaja. 


Mansour Turki, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia amesisitiza kuwa, maeneo ya biashara, masoko na mshirika ya mafuta nchini humo hivi sasa yanakabiliwa na hatari ya kushambuliwa wakati wowote ule.

 Amesema kuwa, hivi sasa polisi ya nchi hiyo inapitia kipindi kigumu mno katika kusimamia usalama ingawa hata hivyo hakutoa maelezo kamili juu ya suala hilo. 

Hii ni katika hali ambayo polisi ya Saudi Arabia imeanzisha operesheni ya kupekuwa magari katika maeneo ya mji mkuu Riyadh, bali hata watu wanaokwenda kuizuru nyumba ya Mwenyezi Mungu al-Kaabah. 

Mwanzoni mwa wiki hii Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia, alitangaza kuwepo uwezekano wa nchi hiyo kushambuliwa na Harakati ya Answarullah ya nchini Yemen kufuatia mashambulizi ya kichokozi yanayoendelea kufanywa na Saudia dhidi ya nchi hiyo jirani ya Kiarabu.

Wananchi Mkoani Morogoro wamuuwa Polisi


Askari mkoani Morogoro akiwa chini baada ya kupigwa na Wananchi wenye asirakali

Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria, aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, ameuawa mchana huu na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.

Tukio hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi.

Mashuhuda wamesema kwamba polisi hao walikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.

Baada ya kuona hivyo, polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi waliwakabili kwa kuwarushia mawe na hivyo kumwua polisi mmoja.


Mawlana Sheikh Jalala: Rajab Ni Mwezi Wa Mwenyezi Mungu

Maulana Sheikh Hemed Jalala akihutubia waumini wa Kiislam, Msikitini Ghadir,Kigogo-Post.






Katika khutba ya Ijumaa iliyotolewa na Maulana Sheikh Hemedi Jalala,  katika Msikiti wa Ghadiir –Kigogo Dar es slaam, Maulana aliwataka waislamu kuheshimu Mwezi huu wa Rajabu kwa kuwa ni mwezi katika Miezi mitukufu katika uislaam, akinukuu hadithi ya mtume (s.a.w.w) alisema “hakika Rajabu ni mwezi wa Mwenyezi Mungu, haukaribii Mwezi wowote kwa utukufu na heshima, kupigana na makafiri ni haraam”.

Aliendelea kusema kuwa Kabla ya Uislaam, makafiri walikua wakiuheshimu kwa kusimamisha vita, na Uislaam kwa kuwa ni dini ya amani ulikuja kuenzi Mwezi huu na mingineyo, Maulana alisikitika kwa kuwaona baadhi ya waislaam wanapigana, na kumwaga damu ya Waislaam wasio na hatia ndani ya mwezi huu, ambapo uislaam umeharamisha vita na uadui katika mwezi huu. Hao wanaobeba bendera ya uislaam, wanapigana ndani ya mwezi wa Rajabu na kuuana, wakati ni haraam .

Akielezea faida za mwezi huu, Maulana alisema: “yeyote atakaefunga siku moja Mtume (s.a.w.w) anasema mtu huyo anastahili radhi za Mwenyezi Mungu, atawekwa mbali na ghadhabu za Mwenyezi Mungu, mlango mmoja katika milango ya motoni utafungwa, na atakaa mbali na moto kwa masafa ya mwaka mmoja”.

Akitaja matukio ya kihistoria ya kiislaam, yaliyotokea katika mwezi huu alisema ”ndugu zangu waislamu Mwezi huu ni mtukufu na fadhila zake ni nyingi mno na una matukio mazito, miongoni mwa matukio hayo ni:
  1. Mwezi Mosi Rajab ilikua ni siku ya mazazi ya Imam wa Tano (5) Muhammad Baqir (as)
  2. Mwezi Tatu Shahada ya Imam wa Kumi  Ali Naqi (as)
  3. Mwezi 13, ni mazazi ya kiongozi wa waumini, imam Alii bin Abii Twalib (as) ambae alizaliwa ndani ya alkaaba tukufu, alizaliwa siku tukufu, tarehe tukufu, mwezi mtukufu na mahala patukufu.
  4. Mwezi 15, shahada ya bi Zainab (as) bint Alii (as) samba wa karbalaa.
  5. Mwezi 25 Pia kuna shahada ya imam musa kadhim (as) na vita ya khaybar
  6. Mwezi 26 ni shahada (kifo ) cha mzee Abii Twalib, baba na mlezi wa mtume Muhammad (s.a.w.w.)
  7. mwezi 27, ni tukio la kihistoria la Israa na Miiraj (safari ya mtume s.a.w.w) kwenda Jerusalem na kisha kwenda mbingu saba, na ni siku aliyopewa utume, mtume Muhammad (s.a.w.w).
    Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa makini katika kusikiliza Hotuba ya Maulana Sheikh Hemed Jalala.

  8. Pia maulana aliwafahamisha baadhi ya dua na aamal za kufanywa katika mwezi huu na akawataka wanaouona mwezi huu ni kama wa kawaida, kuachana na dhana hizo, kwani Mwenyezi Mungu mwenyewe ameutukuza na kuwataka waislaam wauheshimu, vipi wanauona wa kawaida, “ watambue kuwa si Mwezi wa kawaida, bali ni Miongoni mwa miezi Mitukufu una mazuri, matukufu na fadhila nyingi sana kwa watakao uadhimisha.