|
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea katika Semina ya Quds imeyowakusanya Maimam, Masheikh na Maustadhi kutoka madhehbu mbalimbali ya Kiislamu, imeyofanya Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam. |
Kiongozi
Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala ameitaka Jumuiya ya Umoja wa Mataifa (UN) kuiangalia nchi ya Palestina kwa jicho la karibu ili amani iwezekurejea kama ilivyo kwa nchi ya Tanzania.
Sheikh
Hemed Jalala ameyasema hayo leo katika semina ya Quds yenye lengo la kuwakumbuka
waislamu na Wasiokuwa Waislamu wote wanaoishi kwa kupata taabu nchini Palestina, ambapo
ameeleza kuwa watanzania inabidi waoneshwe kusikitishwa na kupinga
vikali dhidi ya mambo yanayoendelea nchini humo kwani kinamama wanakosa
huduma za afya jambo linalopelekea kujifungua kwa taabu.
|
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika Semina ya Quds, imeyowajumuisha Maimam, Masheikh na Maustadhi, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Pot Dar es salaam. |
|
Maimam,Masheikh na Maustadhi wakiwa makini kusikiliza mada mbalimbali zimezowasilishwa katika Semina ya Quds, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam. |
|
Sheikh
Jalala ametaja hali ya hatari inayoikabili msikiti wa AQSWA ambao ni mali ya Waislamu hiyo na kueleza kuwa
hivi sasa Msikiti huo haumilikiwi na waislamu kwa asilimia miamoja pamoja na mali zake, bali unamilikiwa na Utawala Haramu wa Israel, hivyo
umoja wa mataifa ni vyema ikafanyika juhudi kuirejesha haki hiyo kwa
waislamu kwa amani.
"Waislam na wasio waislam wamefukuzwa na Utawala haramu wa Israel katika ardhi yao halali ya Palestina kwani mpaka sasa Wananchi halali ya Palestina
hawaishi kwa amani ambapo hadi nyumba zao zinavujwa na wanafariki kwa
kukosa huduma za afya" amesema Sheikh Jalala
Siku
ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni siku ambayo Waislam, Wasiokuwa Waislamu na Wapenda amani wameiteua kuwa ni siku
maalum ya kuwakumbuka wanyonge wa Palestina na duniani kote na kufikisha ujumbe kwa
dunia kuwa wanahitaji kusaidiwa, hivyo hapa Dar es alaam Tanzania tutakuwa na maandamano maalum
yatakayo anzia maeneo ya Ilala Boma wilaya ya Ilala mpaka katika kiwanja cha Pipo Kigogo Post, Dar es
Salaam.
|
Maimam,Masheikh
na Maustadhi wakiwa makini kusikiliza mada mbalimbali zimezowasilishwa
katika Semina ya Quds, imeyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es
salaam |