Imeelezwa
kuwa mafundisho ya Dini ya kiislamu hayana uhusiano kabisa na matendo
ya kigaini kwani uislamu umejikita kufundisha watu masula ya Amani.
Suala
la dhana iliyojaa katika nafsi za watu kwamba waislamu wanafundisha
uhasama kati ya kundi, mtu ama watu, kuwa wauaji kama inavyotafsriwa na
watu walio wengi ni batili na inalenga kuuchafua uislamu na wafuasi wa
mafundisho ya dini hiyo.
Akizungumza
na ummati wa watu waliohudhuria kikao cha pamoja ya viongozi wa dini
mbalimbali waliokutana kujadili mienendo ya ugani Barani Afriaka,
Kiongozi wa kiroho wa dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA hapa nchini Sheikh
Hemed Jalala alisema lazima umma ufahamu kuwa uislamu haufundishi
ugaidi.
Sheikh huyo alisema kuwa vitendo
vya ugaidi na mauaji yanayofanywa na watu mbalimbali barani Africa na duniani kwa ujumla hayahusiani hata
kidogo na dini ya kiislam kama ilivyokua ikielezwa na wadau mbalimbali.
Sheikh Jalala Ameongeza kusema kuwa ugaidi
katika bara la Africa umekuwa ukitafsiriwa kuwa ni jambo ambalo limekuwa katika
msukumo wa dini ya kiislam jambo ambalo amesema kuwa watanzania wanapaswa
kuelewa sio sahihi kuwatuhumu waislam kwa ugaidi kwani hakuna kitabu chochote
kinachoruhusu muislam kufanya mauaji kwa mwadamu mwenzake.
Amefafanua kuwa
mivutano na Ugaidi uliyopo barani Africa umekuwa ukisababishwa na mambo matatu
ambayo ameyataja kuwa ni ugaidi wa kifikra,kiuwezo na ugaidi wa kudai haki.
Aidha Ameongeza kuwa
dini zote duniani hakuna hata ushaidi wa dini moja ambayo inaruhusu ama
kushabikia vitendo vya mauaji ya kigaidi yoyote yanayotokea afrika..
Katika hatua nyingine
sheikh JALALA akizungumzia swala ambalo limekuwa likitamkwa na serikali kuwa
viongozi wa dini ya kiislam wamekuwa wakiwafundisha vijana wao wa mbinu na njia
za ugaidi ameitaka serikali kuacha kauli hizo kwani ni kauli za kichochezo na
zisizo na ushahidi wowote na badala yake wafwatilie swala hilo kiundani pasipo
kuitaja dini yoyote kuhusika.
Akizungumza katika
kikao hicho muwakilishi wa wakiristo katika mkutano huo pastor PRINCE ERASTO
IKONGO kutoka pentecoste Tabata amesema kuwa viongozi wa dini za kikiristo
wamekuwa na hofu kubwa juu ya ndugu zao ambao ni waislam hofu ambayo
wamejengewa kuwa viongozi wa dini za kiislam pamoja na waumini wao ni watu wa
mauaji na ugaidi jambo ambalo amewatoa wasi wasi wakristo na kuwataka kujenga
umoja na mshikamano juu ya waislam na dini zote Tanzania ili kuidumisha amani
ya nchi.
Amesema kuwa hofu iliyojaa miongoni mwa viongozi wa dini za kikristo ni hofu ambayo imejengwa na wanadamu kuwa waislam ndio wanaohusika na mauaji mbalimbali ambayo yanatokea duniani ya kigaidi jambo ambalo linapaswa kufutika miongoni mwa wakristo ili waweze kudumisha umoja wanchi.
Sehemu ya Umma uliohudhulia kikao hicho |
Amesema kuwa hofu iliyojaa miongoni mwa viongozi wa dini za kikristo ni hofu ambayo imejengwa na wanadamu kuwa waislam ndio wanaohusika na mauaji mbalimbali ambayo yanatokea duniani ya kigaidi jambo ambalo linapaswa kufutika miongoni mwa wakristo ili waweze kudumisha umoja wanchi.