Waislamu na Watanzania nchini wametakiwa kuwaonea huruma yatima na kuwapa huduma bora ikiwemo elimu, afya, malazi kama wanavyowahudumia watoto wao bila
kufanya ubaguzi wa aina yeyote.
Hayo yamesemwa na jana na Mkufunzi wa Chuo cha Kiislamu cha Hawzat Imam
Swadiq Sheikh Ghawth Nyambwa katika futari maalum na mayatima
iliyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Chuo cha Kiislamu (Hawzat) Imam Swadiq (a.s) Sheikh Ghawth Nyambwa akiongea na Waandishi wa Habari katika Futari maalumu ya Yatima, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam. |
Sheikh Ghawth ameeleza kuwa katika maamrisho ya dini ya kiislamu kupitia
kitabu chake kitakatifu kinasema miongoni mwa nyumba bora ni ile
anayoishi yatima na kupewa huduma zinazostahiki, hivyo ni vyema waislamu
kutumia fursa hiyo kwa kuwalea mayatima kwani kuna malipo makubwa kwa
mwenye kufanya hivyo.
Huku akitolea mfano kuwa mtume wao Muhammad (s.a.w.w) amebashiri pepo kwa wale watakao watendea wema mayatima kwa kuwalea vizuri.
Sheikh Mbukuzi akiwasilisha mada juu ya Umuhimu wa kuwasaidia Yatima, katika futari ya pamoja na Yatima, iliyofanyika Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam |
Sheikh Ghawth amefafanua kuwa endapo mtu atakula mali ya yatima ajue
kuna adhabu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu yake, hivyo hakuna budi
kwa muislamu kulinda mali ya yatima.