Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala |
Aya inazungumzia nini?
Aya hii inatidhibitishia na kutueleza ya
kwamba moja katika majina ya mji
mtakatifu wa makka ambapo mahujaji siku chache zijazo watashuka na kuporomoka
katika mji huo, mwenyezimungu(swt) ameuita vilevile ndani ya qur’an Ummul
Quraa( mama wa Vijiji).
Kama kuna kijiji kinafaghari
kubwa kinaweza kukusanya kila aina ya faghari basi kijiji cha Makka, kijiji
kilichopo katika bonde takatifu la Bakka,kijiji hicho ni kijiji ambacho hakina
mfano wake, kijiji hicho ni Ummul Quraa(Mama wa Vijiji).
Suratul Fatihi 24, “Na
Yeye ndiye aliyeizuia mikono yao kwenu, na mikono yenu kwao, katika bonde la
Makka baada ya kukupeni Ushindi juu yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona
myatendayo”
Aya inazungumza
mwenyezimungu vipi amewanusuru waislam na kuwasaidia waislam na kuwaunga mkono
waislam, lakini hayo yametokea wapi? Yametokea katikati ya mji wa makka.
Aya hizi tatu zinatuwekea
barabara ya kwamba Makka inamajina mengi yaliyoitwa ndani ya Qur’an katika
majina hayo ni Bakka,Makka na Ummul Quraa ( Mama wa Vijiji), aya hizi
zinamaelezo marefu lakini kwa kuwa nipo katika maelekezo na katika darsa ya
kubainisha majina ya makka sitoingia kuzisherehesha aya hizo kwa kirefu.
Napenda tuingie katika
Sunna katika Riwayat tuziulize riwayat makka ina majina gani?, mbele yangu hapa
ninayo maneno na hadith ya Imam Ali Ibn Abu Twalib (a.s), Ali Ibn Abutwalib
(a.s) anajibu swali kutoka kwa mtu wa Shamu na anamwabia hivi kwanini makka
imeitwa Ummul Quraa (Mama wa Vijiji),
Qur’an imeita Makka
Ummul Quraa (mama wa Vijiji), huyu mtu anamuuliza Imam Ali Ibn Abutwalib ni
kwani Makka imeitwa Umul Quraa? Imam Ali Ibn Abutwalib anajibu anasemaje
anasema ni kwasababu ardhi imetabaazwa ,imetawanywa chini ya ardhi ya Makka.
Hii ardhi mwenyezimungu(swt)
ameitawanya , mwenyezimungu amelizungumza hili katika qur’an, aya tofauti “Na
ninaapa kwa ardhi na Yule alieitawanya” kwa ibara nyingine adhi ilikuwa ni
donge,MwenyeziMungu(swt) akaitawanya akapasua Mito,bahari ,maziwa, milima na
mabonde. Qur’an imelizungumza hili zaidi ya miaka 1400 iliyopita,
Kwaivyo kwa kuwa ardhi imetawanywa
chini ya makka ndio likafanya mji wa makka uitwe Ummul Quraa (Mama wa Vijiji)
kwa sababu ni mama wa miji yote,ni mama wa vijiji vyote na ndio katikati ya
nchi zote.
Imam ali (a.s) anasema
kunatofauti gani ya Makka na Bakka? Iko wapi makka na bakka, makka ni ile
kalafu,ni ile kandokando ya haraam huwenda mtu ukatatizika kwamba mbona qur’an
mara inasema Bakka, wakatimwingine inasema Makka mbona inatuchanganya Qur’an ,
wakati mwingine inaita Umul quraa mbona hatuielewi.
Na leo dunia watu
wamesumbuka na watasumbuka, kwanini, kwasababu Yule anaeijua qur’an watu
wamemuacha na siku zote na jamii yoyote ikimkamata huyu anaeijua quran na
tafsiri ya quran lazima inyoke,lazima ifanikiwe.
Sasa ametueleza ali
kwanini imeitwa Bakka na Umul quraa amesema Makka ni kandokando ya haram na Baka
ni pale ilipo al-kaaba,kwanini imeitwa Maka kwa sababu mwenyezimungu(swt) hii
ardhi ilikuwa donge, mungu akaitawanya kutoka chini ya makka. Na ndio
katikakati na ndio wanapoelekea waislam wote katika swala zao, katika dua zao
hata wanaposoma Qur’an.
Na huyu kiongozi atakaeleta
amani duniani na maelewano duniani na kusikilizana na kupendana na dunia yote
kuwa ni mahala pa maelewano chini ya bendera ya Lailaha ilallah, Muhammadun
Rasulullah, mtu huyu kudhihiri kwake itakuwa siku ya ijumaa.Faraja,
kheri,neema,ushindi utapatikana kwa hiyo siku atakapo dhihiri mahala hapo ni
makka,atakapodhiri hapo watu watakwenda kwa magoti kumtii(kumpa baiya) Imam
Mahd (a.s).
Sasa kwanini imeitwa
Bakka kwa sababu Makka imewaliza majabari watu wenye kibri, watu wenye
madhambi, watu wenye makosa , ukijifanya unakibri na ukaenda makka na Ukataka
kuishambulia basi utarudu unalia na ndivyo ilivyotokea kwa mfalme Abraha wakati
alipolituma jeshi lake kwenda kuivunja Al-kaaba.
Mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala |
Abulmutwalib ndio
muhusika wa makka akaenda kwa mfalme na akamwambia mfalme wanajeshi wako
walipokuja walichukua mbuzi zangu ,hivyo naomba mbuzi zangu uzirudishe, mfalme
akashangaa, akasema badala ya kuniomba nisivunje Al-kaaba unaniomba mbuzi,
Abdulmutwalib akasema ile nyumba inamwenyewe, aliporudi Abraha akatuma jeshi,
jeshi linaongozwa na Tembo.
Abdulmutwalib akawambia
watu wa makka kimbieni milimani jeshi linakuja, wakakimbia, kisha akaenda
kukamata kamba ya Al-kaaba akamwambia mungu (swt) nyumba hii ni nyumba yako
ilinde nyumba yako inakuja kushambuliwa na kuvunjwa leo.
Akaacha nae akaondoka
kwenda kujificha, kilichotokea mwenyezimungu (swt) anamajeshi mengi.Mungu
anamajeshi kila mahala ya ardhi na mbinguni, Abraha anakuja kuvunja al-kaaba
anafika hatua chache tu, Allah (swt) anawapeleka ndege wamekamata vidongo
kwenye midomo yao ,vidogo vile vilikuwa na risasi wakaviachia vidongo ikawa
kidongo kikikupata kwenye kichwa kinatokea chini,mwenyezimungu(swt)
anasema wakabadilika wale watu na
wakasambaratika wakawa kama vile majani yaliyotobolewa tobolewa na wadudu.
Na akabakia mmoja
kaenda kutoa habari, habari hizi zikasambaa dunia nzima ya warabu watu wakazidi
kuiogopa Makka ,ni mahala pasipo pa kawaida na ni mahala tunasoma kila siku
ndani ya Qur’an takatifu ,inshaallah mwenyeimungu(swt) atupatie nguvu tukafanye
haji hiyo makka takatifu.
“Kwani hukuona jinsi
Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?, Kwani
hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?, Na akawapelekea ndege
makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,
Akawafanya
kama majani yaliyo liwa! , Surat A-fiil.
Sasa yoyote anaecheza
na makka adui hana mwisho mzuri atasambaratika , yoyote anacheza na makka
akaifanya maka sio mahala pa amani
akaifanya makka ni ardhi ya ufisadi na kuwapiga watu wasiokuwa na hatia ajue yakwamba atalia siku moja na siku si
nyingi atalia.
Kwanini makka imeitwa
bakka ni kwasababu maka inawaliza au iliwaliza au inatabia ya kuwaliza, kuliza
macho ya wale wenyekujifanya wakubwa na wenye madhambi.ukileta madhambi yako
pale makka utasambaratishwa , ukiifanya maka haiku katika amani, jua hauna
mwisho mzuri.
Bakka ni pale mahala ilipo
al-kaaba na hakika makka ni haraam,mwenyekuiingia basi yupo katika amani, makka
ni pale harram ambapo ni masafa makubwa , al-kaaba ni sehemu ndogo tu,lakini
mahala panapoitwa harram ni mahala papana mmno. Mtu kama amefanya matatizo yake
anataka kuuwawa akiingia pale yupo katika amani, mnyama anafukuzwa huko anataka
kuuwawa akiingia pale yupo katika amani,njiwa wa pale huruhusiwi kumgusa
Ninawaambia waislam
kumbe Dini yao sio imeweka miezi Fulani minne ni miezi ambayo huruhusiwi watu
kupigana na kumwaga damu, hapana bali uislam umeweka ardhi maalum ambayo ardhi
hiyo aina yoyote ya kiumbe haruhusiwi kuuwawa na kumwaga damu yake.
Uislam wa kuuwana unapatikana
wapi?Uislamwa kuchinjana unapatikana wapi?,kumbe uislam sio umetaja miezi tu
yakuwa katika amani, hapana bali Uislam umetaja sehemu, sehemu hiyo hatadamu ya
Kunguni ni hairuhusiwi kumwagwa, hata mbu huruhusiwi kumuua, bali unatakiwa
kumuondoa kwa heshima na adabu na ukimuua unatakiwa uchinje Kondoo mzima ya
Kafara.Itaendelea...