Tuesday, June 9, 2015

Polisi yawatawanyisha CHADEMA kwa mabomu.

Jeshi la polisi wilayani Iramba limetumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuwakamata Mwenyekiti wa uhamashishaji kanda ya kati Bi Jesca Kishoa na katibu wa BAVITA wilayani Iramba Bwana Rayman Minja, wakati walipokuwa wakiwahamasisha wananchi kwenye mkutano wa hadhara kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.(P.T)
Akieleza baada ya kuachiwa na jeshi la polisi alipokuwa amewekwa chini ya usalama kwa zaidi ya masaa matano mwenyekiti wa uhamashishaji CHADEMA kanda ya kati Bi. Jesca Kishoa, amesema anashangaa kuona Mkuu wa Wilaya ya Iramba akiwakataza kufanya mikutano huku vyama vingine vimekuwa vikifanya mikutano, jambo ambalo hastahili kufanya hivyo kwa sababu yeye anatawala wananchi wenye vyama tofauti na siyo chama kimoja.
Kwa upande wao, wananchi wa wilaya ya Iramba wametupia lawama kwa jeshi la polisi kuzuia mikutano minne ya CHADEMA, pia kutumia nguvu kutawanya watu kwa kuwa mwagia maji ya kuwasha na kuwapiga mbomu ya machozi.
Akionge kwa simu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida, Bwana Thobias Sedoyeka amesema wao wanatekeleza amri ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba ya kupiga marufuku na kuzuia maikutano yoyote ya hadhara ifanyike wilayani humo.

                                                           Taarifa via ITV                   

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei 2015 umeongezeka

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es salaam.Mfumuko wa Bei wa bei kwa mwezi Mei,2015 umefikia asilimia 5.3 kutoka asilimia 4.5 iliyokuwepo mwezi Aprili, 2015.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei 2015 umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.3 kutoka asilimia 4.5 ya mwezi Aprili 2015 kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema kuwa kuongezeka kwa mfumuko wa Bei nchini kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa za vyakula zinazotumiwa kwa wingi na kaya binafsi kwa mwezi Mei.
Amesema bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo ni Nyama,Choroko, Maharage,samaki, nyama,unga wa mihogo.
Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni bei za mavazi ya wananume kwa asilimia 5.6, mavazi ya wanawake kwa asilimia 3.5, vyakula kwenye migahawa kwa asilimia 4.1 na huduma za malazi kwa asilimia 4.2.
Kuhusu Fahirisi za bei kwa maana ya namna bei zinavyopanda kutoka kipindi kimoja hadi kingine kwa mwezi Mei zimeongezeka hadi kufikia 157.86 kutoka 157.21 za mwezi Aprili 2015 kutokana kuongezeka kwa bei ya bidhaa za vyakula ambazo ni mahindi, unga wa mahindi, samaki wabichi, ndizi ,mbogamboga,viazi mviringo ,maharage na mihogo.
Kwa upande wa baidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa Fahirisi za bei kwa kipimo cha mwezi Kwesigabo amesema kuwa Mafuta ya Dizeli ambayo yamechangia kwa asilimia 3.2 na na mafuta ya Petroli kwa asilimia 5.8.
Aidha,kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Mei , 2015 amesema umefikia shilingi 63 na senti 35 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 63 na senti 61 za mwezi Aprili 2015.
“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Mei ,2015 na Aprili ,2015 umepungua, hii inamaanisha sasa mtu anahitaji kuongeza ziada ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Mei"
Kwa upande wa mfumuko wa Bei wa mwezi Mei 2015 kwa nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 6.87 na kutoka 7.08 mwezi Aprili,2015 huku Uganda mfumuko wa bei kwa mwezi Mei ,2015 ukiongezeka hadi asilimia 4.90 kutoka asilimia 3.60 za mwezi zilizokuwepo mwezi Aprili, 2015.(Muro)

'Uingereza, Marekani zinaunga mkono ugaidi Kenya'


Serikali ya Kenya imezituhumu Uingereza, Marekani, Norway na Finland kuwa zinaunga mkono ugaidi wa kundi la al Shabab kwa kutoa misaada kwa mashirika ya kijamii yanayoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi hilo.
Katika barua ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya kwa balozi za nchi hizo mjini Nairobi, serikali ya Kenya imezitaka nchi hizo za Magharibi kusitisha mara moja misaada yao kwa mashirika hayo ya kijamii hasa kwa shirika la Haki Africa na Shirika la Waislamu Watetezi wa Haki za Binadamu (Muhuri).
Mashirika hayo mawili yenye makao yao mjini Mombasa ni kati ya mengine 85 ambayo serikali ya Kenya inasema inaamini yanafadhili ugaidi wa al Shabab nchini humo.

Katika taarifa hiyo, serikali ya Kenya imesema, katika hali ambayo serikali hizo za kigeni zinasema zinaisaidia Kenya kupambana na ugaidi lakini kuna ishara kuwa zinafanya kinyume ya hilo kwa kuchochea moto wa ugaidi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya, Mwenda Njoka amesema baadhi ya mashirika hayo ya kijamii yamejitokeza wazi na kuwasaidia washukiwa wa ugaidi kwa kuwapa mawakili. 
Hata hivyo wakuu wa Muhuri na Haki Africa wamekanusha madai ya serikali ya Kenya kuwa wanaunga mkono ugaidi nchini humo.
Chanzo:Irbi