Serikali ya Kenya imezituhumu Uingereza, Marekani,
Norway na Finland kuwa zinaunga mkono ugaidi wa kundi la al Shabab kwa kutoa
misaada kwa mashirika ya kijamii yanayoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi hilo.
Katika barua ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya kwa balozi za nchi hizo mjini Nairobi, serikali ya Kenya imezitaka nchi hizo za Magharibi kusitisha mara moja misaada yao kwa mashirika hayo ya kijamii hasa kwa shirika la Haki Africa na Shirika la Waislamu Watetezi wa Haki za Binadamu (Muhuri).

Mashirika hayo mawili yenye makao yao mjini Mombasa
ni kati ya mengine 85 ambayo serikali ya Kenya inasema inaamini yanafadhili
ugaidi wa al Shabab nchini humo.
Katika taarifa hiyo, serikali ya Kenya imesema,
katika hali ambayo serikali hizo za kigeni zinasema zinaisaidia Kenya kupambana
na ugaidi lakini kuna ishara kuwa zinafanya kinyume ya hilo kwa kuchochea moto
wa ugaidi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya, Mwenda
Njoka amesema baadhi ya mashirika hayo ya kijamii yamejitokeza wazi na
kuwasaidia washukiwa wa ugaidi kwa kuwapa mawakili.
Hata hivyo wakuu wa Muhuri
na Haki Africa wamekanusha madai ya serikali ya Kenya kuwa wanaunga mkono
ugaidi nchini humo.
Chanzo:Irbi
No comments:
Post a Comment