Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Katibu mkuu wa Jumuiya ya
kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema Jumuiya hiyo inayoongozwa na
Marekani imekamilisha mipango ya kikosi cha hatua ya haraka cha hadi
wanajeshi 40,000 , mara mbili zaidi ya idadi ya sasa, pamoja na ofisi
mapya za makaao makuu ya NATO nchini Hungary na Slovakia. Uamuzi huo
umechukuliwa katika mkutano wa Mawaziri wa ulinzi wa NATO leo mjini
Brussels, ambao uligubikwa na wasiwasi wa hatua za kijeshi za Urusi
hivi karibuni nchini Syria. Kwani jumuia hiyo imekuwa ikiwaunga mkono
waasi na magaidi wanaofanya jinai nchini Syria na Iraq kwa malengo yao
machafu ya kisiasa.
Alisema uamuzi huo unatuma ujumbe kwa raia wote wa nchi za NATO
kwamba Jumuiya hiyo itawalinda, ipo na iko tayari. Akizungumza hapo
kabla kuhusu kujiingiza kijeshi Urusi nchini Syria, alisema Urusi
haiwashambulii tu waasi wa Dola la Kiislamu lakini pia makundi mengine
ya waasi na magaidi yanayoungwa mkono na jumuia hiyo yanayoupinga
utawala wa Assad . Stolenberg akatoa wito kwa Urusi akisema:
"Ninatoa wito kwa Urusi itowe mchango madhubuti na wa ushirikiano
katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh tu na sio kuendelea kuwaua magaidi
wa vikundi vingine na kuunga mkono utawala wa Assad. Kwa sababu huo
sio mchango madhubuti kuelekea suluhisho la amani na la kudumu nchini
Syria."chanzo abna24