Sunday, July 12, 2015

QUDS ni siku ya Amani


Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habari katika Matembezi ya Aamani ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

 Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waisla Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema Siku ya Quds ni siku ya amani, ni siku ya kunyanyua sauti dhidi ya Dhulma, dhidi ya watu ambao hawana uhuru.
“Nasema ni siku ya amani kwasababu siku hii ya leo ilitangazwa kimataifa kwamba ni siku ya kukumbuka matatizo yanayowakumba ndugu zetu walioko katika ardhi ya Palestina...
Kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Shekh Hemed Jalala akigawa bendera za tanzania na palestina kama ishara ya kuanza rasmi kwa matembezi hayo  jijini Dar es salaam.
Inatambuluka ya kwamba ardhi ya palestina ni ardhi iliyokaliwa kwa mabavu ni ardhi iliyokaliwa pasina ridhaa ya wenyewe, wapalestina wakafukuzwa katika nchi yao ambayo ndio nchi yao ya Asili.
Naleo hii tukiwazungumza wapalestina hawa kama wanaadamu wenzetu wapo katika nchi tofauti wamegawanyika duniani, gurupo wapo mashariki ya kati wengine wapo nchi za ulaya, bali hata katika nchi zetu za afrika,watu hao wamejaa” alisema Sheikh Jalala. 
Jalal alisema Kitendo cha wao kutoishi katika nchi yao ni kitendo ambacho sisi kama Viongozi wa dini, sisi kama watanzania, sisi kama wadu wa amani ni jambo tunaona kwamba kwa kulinyamazia  sio mahala pake na ni jambo ambalo sio la kisawasawa.
“Tunasema ya kwamba ni haki ya mwanaadamu yoyote kuishi kwa amani na utulivu katika nchi yake, kuzungumza anachoweza kukizungumza,kula na kuishi kama mwanaadamu mwingine, haya yote yamekosekana kwa watu wa palestina.
Waumini wa Dini ya Kiislam na Kiikristo Pamoja na Wapenda amani Duniani wakiungana katika matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya quds
Siku hii ya leo ndugu zangu ni siku ambayo tunakumbuka sote duniani ya kwamba kama itakosekana amani, basi busara itakosekana, hekima itakosekana, na utulivu utakosekana. Sisi kama Watanzania ni haki yetu kuwaunga mkono wapalestina na kuwaombea mungu kwamba amani iwepo kama iliopo hapa Tanzania, alisema Sheikh Jalala
Aliongeza kuwa Kama ilivyokuwa Tanzania ni mahala pa amani hapamtofautishi mwislam wala mkristo watu wote tumekaa pamoja, amani hii, maelewano haya na utulivu huu , siku hii ya Quds tunaomba Palestina iwe katika hali hiyo na iwe katika mazingira hayo.
Kitendo cha Dhulma kilichowakumba Wapalestina sisi kama watanzania  ni haki yetu kisimama na kusema ya kwamba, kwa kuwa mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere Mwasisi wa Taifa hili alikuwa mtu wa kwanza kuupinga dhulma na Uvamizi wa Palestina.