Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Waislam, Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Mawlana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habari katika Matembezi ya Aamani ya Siku ya Kimataifa ya Quds. |
Kiongozi Mkuu wa Kiroho
wa Waisla Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema
Siku ya Quds ni siku ya amani, ni siku ya kunyanyua sauti dhidi ya Dhulma, dhidi
ya watu ambao hawana uhuru.
“Nasema ni siku ya
amani kwasababu siku hii ya leo ilitangazwa kimataifa kwamba ni siku ya
kukumbuka matatizo yanayowakumba ndugu zetu walioko katika ardhi ya Palestina...
Kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Shekh Hemed Jalala akigawa bendera za tanzania na palestina kama ishara ya kuanza rasmi kwa matembezi hayo jijini Dar es salaam. |
Inatambuluka ya kwamba
ardhi ya palestina ni ardhi iliyokaliwa kwa mabavu ni ardhi iliyokaliwa pasina
ridhaa ya wenyewe, wapalestina wakafukuzwa katika nchi yao ambayo ndio nchi yao
ya Asili.
Naleo hii tukiwazungumza
wapalestina hawa kama wanaadamu wenzetu wapo katika nchi tofauti wamegawanyika
duniani, gurupo wapo mashariki ya kati wengine wapo nchi za ulaya, bali hata
katika nchi zetu za afrika,watu hao wamejaa” alisema Sheikh Jalala.
Jalal alisema Kitendo
cha wao kutoishi katika nchi yao ni kitendo ambacho sisi kama Viongozi wa dini,
sisi kama watanzania, sisi kama wadu wa amani ni jambo tunaona kwamba kwa
kulinyamazia sio mahala pake na ni jambo
ambalo sio la kisawasawa.
“Tunasema ya kwamba ni
haki ya mwanaadamu yoyote kuishi kwa amani na utulivu katika nchi yake,
kuzungumza anachoweza kukizungumza,kula na kuishi kama mwanaadamu mwingine,
haya yote yamekosekana kwa watu wa palestina.
Waumini wa Dini ya Kiislam na Kiikristo Pamoja na Wapenda amani Duniani wakiungana katika matembezi ya amani ya siku ya kimataifa ya quds |
Siku hii ya leo ndugu
zangu ni siku ambayo tunakumbuka sote duniani ya kwamba kama itakosekana amani,
basi busara itakosekana, hekima itakosekana, na utulivu utakosekana. Sisi kama
Watanzania ni haki yetu kuwaunga mkono wapalestina na kuwaombea mungu kwamba
amani iwepo kama iliopo hapa Tanzania, alisema Sheikh Jalala
Aliongeza kuwa Kama ilivyokuwa
Tanzania ni mahala pa amani hapamtofautishi mwislam wala mkristo watu wote
tumekaa pamoja, amani hii, maelewano haya na utulivu huu , siku hii ya Quds
tunaomba Palestina iwe katika hali hiyo na iwe katika mazingira hayo.
Kitendo cha Dhulma
kilichowakumba Wapalestina sisi kama watanzania
ni haki yetu kisimama na kusema ya kwamba, kwa kuwa mwalimu Juliasi
Kambarage Nyerere Mwasisi wa Taifa hili alikuwa mtu wa kwanza kuupinga dhulma
na Uvamizi wa Palestina.
No comments:
Post a Comment