Friday, May 1, 2015

Madrasa ni Muhimili katika Jamii bora

Sheikh. Hemde Jalala akitoa hotuba katika swala ya Ijumaa, Msikitini Ghadir, Kigogo-Post, Dar es salaam

Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa makini kusiiliza hotuba ya swala ya Ijumaa kutoka kwa Maulana Sheikh Jalala




Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Ghadir Maulana Hemed Jalala ametoa wito kwa Taifa la Tanzania kama linahitaji watumishi wenye maadili mema ni lazima kuzienzi Madrasa.


Hayo ameyasema leo katika swala ya Ijumaa,Msikitini Ghadir, Kigogo-Post, jijini Dar es salaam.


Maulana Jalala amesema Madrasa ni mahali panapo walea watoto wenye maadili ya K-mungu, penye msingi wa kuwakataza wasiwe waongo, wasichukue rushwa, wasifuje mali za umma.


Aidha Maulana Jalala amesema kuwa Madrasa sio adui wa Nchi bali ni kipenzi na mlezi wa Nchi katika kupambana na walarushwa na wenye kufuja mali za umma.


Ametoa pandekezo kwa Wizara ya Elimu kuwa ni halali Wizara ya Elimu kuwafikiria Walimu wa Madrasa kwa kuwapatia Mishahara kama Walimu wengine wanaofanya kazi kwa ajili ya umma kwa kuilea jamii katika maadili mema.

 “Taifa hili kama lina hitajia kuifunga Taasisi ya Takukuru, kupata wakusanyaji kodi wazuri, rai wema na wasio waovu, na wala Rushwa basi ni kuzienzi madrasa, na akaitaka wizara ya elimu kuzienzi madrasa hizo na kuzitia nguvu kwa kuzipa posho kwani kazi zinazofanya zina mchango mkubwa kwa jamii na kwa Taifa kwa ujumla." Amesema Sheikh Jalala.