Sheikh. Hemde Jalala akitoa hotuba katika swala ya Ijumaa, Msikitini Ghadir, Kigogo-Post, Dar es salaam |
Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa makini kusiiliza hotuba ya swala ya Ijumaa kutoka kwa Maulana Sheikh Jalala |
Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Ghadir Maulana Hemed
Jalala ametoa wito kwa Taifa la Tanzania kama linahitaji watumishi wenye
maadili mema ni lazima kuzienzi Madrasa.
Hayo ameyasema leo katika swala ya Ijumaa,Msikitini
Ghadir, Kigogo-Post, jijini Dar es salaam.
Maulana Jalala amesema Madrasa ni mahali panapo
walea watoto wenye maadili ya K-mungu, penye msingi wa kuwakataza wasiwe waongo,
wasichukue rushwa, wasifuje mali za umma.
Aidha Maulana Jalala amesema kuwa Madrasa sio adui
wa Nchi bali ni kipenzi na mlezi wa Nchi katika kupambana na walarushwa na
wenye kufuja mali za umma.
Ametoa pandekezo kwa Wizara ya Elimu kuwa ni halali
Wizara ya Elimu kuwafikiria Walimu wa Madrasa kwa kuwapatia Mishahara kama
Walimu wengine wanaofanya kazi kwa ajili ya umma kwa kuilea jamii katika
maadili mema.
“Taifa hili kama lina hitajia kuifunga Taasisi ya Takukuru, kupata wakusanyaji kodi wazuri, rai wema na wasio waovu, na wala Rushwa basi ni kuzienzi madrasa, na akaitaka wizara ya elimu kuzienzi madrasa hizo na kuzitia nguvu kwa kuzipa posho kwani kazi zinazofanya zina mchango mkubwa kwa jamii na kwa Taifa kwa ujumla." Amesema Sheikh Jalala.

No comments:
Post a Comment