Mbunge
Godbless Lema amerejeshwa tena rumande leo baada ya rufaa yake ya
kupinga kunyimwa dhamana kushindikana kusikilizwa kama ilivyokuwa
imepangwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Jana.
Rufaa
hiyo ya Lema iliyokuwa umepangwa kusikilizwa leo imeshindikana baada ya
upande wa Jamhuri kukata rufaa kupinga kuongezwa muda wa kuwasilisha
notisi ya rufaa.
Mawakili
wa Lema waliomba kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa
kupinga kunyimwa dhamana baada ya kushindwa kufanya hivyo katika muda
uliokuwa umepangwa awali.
Jaji
aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa
mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi
upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 Disemba 2016 ambapo tarehe 2
Januari watakutana pande zote kwa ajili ya kufanya majumuisho na
maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 Januari 2017.
Mbunge
Godbless Lema ambaye alikamatwa Novemba 2 mwaka huu mjini Dodoma
amerejeshwa rumande katika gereza la Kisongo jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment