Monday, February 1, 2016

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi -Sehemu ya Pili

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiAssalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi na karibuni kuwa nasi katika mfululizo huu wa vipindi maalumu vinavyokujieni kwa mnasaba wa maadhimisho ya Alfajiri Kumi ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambapo leo tutayazungumzia Mapinduzi ya Kiislamu, kama kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi. Endeleeni kuwa nami hadi mwisho wa kipindi kusikiliza niliyokuandalieni katika mfululizo huu.

Amma taathira ya tatu ya Mapinduzi ya Kiislamu imetokana na kulinda thamani na tunu za Kiislamu. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kinyume na mapinduzi mengi yaliyotokea duniani, hayakukengeuka njia yake ya asili, na hayakuwa tayari kwa hali yoyote ile kuachana na thamani zake aali na malengo yake matukufu licha ya vizuizi na mashinikizo ya kila namna yaliyokabiliana nayo. 

Kwa sababu hiyo, Mapinduzi ya Kiislamu yamekuwa ni nembo ya harakati ya kupigania haki katika uga wa maisha ya kisiasa na kijamii.

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiMUZIKI
Mapinduzi ya wananchi wa Iran yalikuwa na mvuto mkubwa kwa mataifa mengine katika sura tofauti; na kutokana na kuwa tajiriba moja mpya iliyotokana na thamani za kidini na kiutu yalitoa ilhamu kwa harakati na mabadiliko ya ulimwengu na kwa mageuzi ya kijamii.

Kabla ya kujiri Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kwa kuzingatia kutawala duniani fikra mbili za Ubepari na Ukomunisti ilijengwa dhana kwamba mifumo ya tawala haingeweza kutoka nje ya mduara wa moja ya mifumo miwili ya Demokrasia ya Kiliberali na Usoshalisti; na kwa hivyo kama yangetokea mapinduzi yoyote yale duniani yangekuwa hayana budi kuegemea kwenye mhimili wa moja ya fikra mbili hizo na kutegemea msaada na uungaji mkono wa moja kati ya kambi mbili kuu za Mashariki na Magharibi. 

Kwa mintaarafu ya hayo wana nadharia wengi wa Mapinduzi walitaka kuyahakiki Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika kalibu ya moja ya fikra mbili hizo, katika hali ambayo vuguvugu la mapinduzi hayo hadi ushindi wake, pamoja na harakati yake na malengo yake vimejipambanua kikamilifu na fikra hizo.

Ukweli ni kwamba thamani na umuhimu wa mapinduzi yoyote vinategemea ghaya na malengo makuu yanayofuatiliwa na mapinduzi hayo. Ukubwa na udogo wa malengo hayo huwa unachangia kwa kiwango kikubwa gharama ambazo kila mapinduzi yanalazimika kuzilipia. Kadiri malengo ya mapinduzi yanapokuwa na utukufu na mvuto mkubwa zaidi ndivyo yanavyolazimika kuhimili na kuvumilia tabu, misukosuko na mashinikizo makubwa zaidi ili kuweza kuyafikia malengo hayo.

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiMashinikizo na misukosuko ambayo Mapinduzi na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu umeihimili na kuivumilia katika muda wa miaka 38 iliyopita ni ithbati na ushahidi wa kuthibitisha ukweli huu, kwamba ili kufikia ghaya na malengo yake matukufu, taifa la Iran limesimama imara kukabiliana na mashinikizo yote; na kigezo cha kusimama imara huko ni kukataa ubeberu wa madola makubwa duniani na mfumo uliojengwa kwa msingi wa ubabe na utumiaji mabavu, udhalilishaji watu na ubaguzi wa rangi. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalidhihiri na kuasisi mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kwa madhumuni ya kufikia malengo hayo.

MUZIKI
Historia ya Mapinduzi ya Kiislamu inaonyesha kwa uwazi kabisa sababu kuu ya uadui wote huu na njama zote hizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwemo Vita vya kulazimishwa na vikwazo vya uchumi; nayo ni hofu ya taathira za mapinduzi hayo na kuwa kigezo cha kuigwa na wananchi wa mataifa mengine.

Uistikbari wa dunia ambao ulihisi umepoteza maslahi na manufaa yake ya kimaada kutokana na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ulianzisha fitna na njama mara baada ya ushindi wa mapinduzi hayo kwa dhana kwamba utaweza kuyasimamisha, kuyapotosha muelekeo wake na hatimaye kuyasambaratisha. Na ndiyo maana uliamua kukabiliaana na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu; lakini haukupata tija nyengine ghairi ya kushindwa na kugonga mwamba.

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiMhimili mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni nafasi na mchango wa wananchi. Wananchi wa Iran waliendesha mapambano ya muda mrefu na kuweza kuusambaratisha utawala kibaraka wa Kifalme na kuasisi Mfumo wa Kiislamu. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameweza baada ya miaka mingi kuuondoa Uislamu na jamii za Kiislamu kwenye hali ya kutengwa. 

Yakiwa mithili ya injini isukumayo merikebu, yametoa msukumo wa mwamko kwa harakati za Kiislamu na uelewa kwa wananchi wa mataifa ya Kiislamu ya eneo wa kutambua haki zao na uwezo walionao. Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa fikra za kisiasa za Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimetokana na msingi wa mapambano katika njia ya kutetea haki na uadilifu. 

Ni kwa sababu hiyo, ndiyo maana Uistikbari wa dunia ukiongozwa na Marekani uliamua tokea awali kulipa kipaumbele cha kwanza katika sera zake suala la kukabiliana na Mapinduzi ya Kiislamu ili kwa mawazo yake uuangushe Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Katika muda wote wa miaka 38 iliyopita, Marekani imekuwa ikichukua kwa sura ya mtawalia hatua za kiadui na kihasama dhidi ya taifa la Iran. Lakini muqawama wa taifa hili na kusimama kwake imara kumetoa somo na funzo kubwa kwa maadui zake.

Harakati hii adhimu iliyoandamana na muqawama na kusimama imara kuyakabili mashinikizo imesababisha kujiri mageuzi makubwa katika mahusiano ya Iran na ulimwengu wa nje. Ni kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu 
 Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kwamba kukithiri kwa vitisho ni ishara ya kuwa na nguvu Mfumo wa Kiislamu; kwa sababu kama Jamhuri ya Kiislamu ingekuwa haina nguvu na ushawishi wenye taathira, wasiolitakia mema taifa la Iran wasingehaha na kuchacharika kiasi hiki katika kupanga na kutekeleza kila aina ya njama dhidi ya taifa hili.

Wasikilizaji wapenzi kipindi chetu hiki maalumu cha Alfajiri Kumi kimefikia tamati. Ni matumaini yangu kuwa mumenufaika na yale mliyoyasikia katika kipindi hiki. Msiache kujiunga nasi tena katika mfululizo ujao wa vipindi hivi. 

Nakuageni basi huku nikikutakieni usikilizaji mzuri wa sehemu iliyosalia ya matangazo yetu

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi -Sehem ya Kwanza

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiAssalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi na karibuni kuwa nasi katika mfululizo huu wa vipindi maalumu vinavyokujieni kwa mnasaba wa maadhimisho ya Alfajiri Kumi ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambapo leo tutayazungumzia Mapinduzi ya Kiislamu, kama kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi. Endeleeni kuwa nami hadi mwisho wa kipindi kusikiliza niliyokuandalieni katika mfululizo huu.

MUZIKI
Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ni moja ya matukio makubwa zaidi ya karne ya 20; na likiwa moja ya matukio yasiyo na mfano wake katika zama hizi yalifungua ukurasa mpya katika historia ya mwanadamu na kuwa chemchemi ya mabadiliko makubwa katika nyuga za kiutamaduni, kisiasa, kijamii na kiuchumi. 

Mapinduzi ya Kiislamu kwa wananchi wa Iran lilikuwa ni hitajio na jambo la lazima, ambalo liligeuka kuwa mwanzo wa harakati mpya katika uga wa muqawama wa mataifa, katika kukabiliana na mifumo na tawala za kibeberu. Na ndiyo maana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulikuwa ni tukio ambalo mwangwi wake ulivuka mpaka wa kieneo.

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiKimsingi, kila Mapinduzi yanayojiri katika eneo la kijiografia la watu huwa na athari na kusababisha mageuzi na mabadiliko ya msingi; lakini kitu kinachoyalinda mapinduzi hayo na kuyafanya yadumu ni upana na ukubwa wa taathira zake.

 Sifa hii imeonekana kwa uwazi kabisa na kwa kiwango kikubwa katika Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran; kiasi kwamba mataifa mengi ya wanyonge duniani yalihisi kuwa yataweza kupata matamanio na matarajio yao kwa kufuata kigezo cha Mapinduzi ya Kiislamu. 

Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulivuruga mlingano uliokuwa ukitawala katika mfumo wa kisiasa wa kieneo na kimataifa; na kwa kutegemea msingi wa "nguvu ya wananchi" na "kupigania kujitawala" ukafanikiwa kuonyesha mfano wa kukabiliana na siasa za kibeberu. 

Kwa msingi huo, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ulizingatiwa na kupewa umuhimu kutokana na kuwa chemchemi ya kutoa ilhamu kwa mataifa yanayopigania uhuru na kujitawala duniani; na hadi leo hii pia licha ya kupita karibu miongo minne, yangali yanatoa ilhamu kwa harakati za kimapinduzi katika nchi mbalimbali.

Kwa mtazamo wa wana nadharia wa Mapinduzi yaliyojiri duniani, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yana taathira tatu muhimu na za kudumu; na ndiyo sababu iliyoyafanya madola ya kiistikbari yachacharike na kuhaha kwa ajili ya kukabiliana na mapinduzi hayo. 

Taathira ya kwanza na muhimu zaidi ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ilikuwa ni kutoa changamoto kwa mfumo wa Ubeberu duniani. Kwa ushindi wake wenye lengo maalumu, mapinduzi haya yalionyesha kuwa hata kama taifa litakuwa mikono mitupu bila ya kuwa na silaha yoyote, linao uwezo wa kuwa chachu ya kuleta mabadiliko makubwa hata katika mlingano na mahesabu ya madola makubwa duniani. 
Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi
Taathira ya pili ni kwamba Mapinduzi ya Kiislamu yalionyesha nguvu na uwezo halisi wa taifa la watu bila ya kutegemea msaada na uungaji mkono wa lolote kati ya madola makuu ya dunia wakati huo. Na hiyo ndiyo sababu iliyoyafanya Mapinduzi ya Kiislamu yawe ni msukumo wa kujiri mageuzi makubwa ya kisiasa katika upeo wa ulimwengu mzima. 

 Mageuzi na mabadiliko hayo yaliwaonyesha walimwengu nguvu kubwa na uwezo wa kisiasa wa dini ya Uislamu na kuhuisha harakati adhimu ya kujikomboa na ubeberu na kusimama imara kukabiliana na ukoloni.

Umoja, chanzo cha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Umoja, chanzo cha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu ya Iran amesema, umoja wa taifa la Iran ndio sababu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuangushwa utawala wa kifalme wa Pahlavi.

Ayatullah Ali Akbar Hashemi Rafsanjani ameyasema hayo katika sherehe za kukumbuka siku aliporejea nchini Iran Imam Khomeini MA katika uwanja wa ndege wa Mehrabad mjini Tehran. Ameongeza kuwa aghalabu ya watu wa Iran walitaka Mapinduzi ya Kiislamu na kwa umoja wao waliweza kuuangusha utawala wa Shah Pahlavi.

Ayatullah Rafsanjani ameendelea kusema kuwa, taifa la Iran linapaswa kuendeleza harakati za kufikia malengo matukufu ya Imam Khomeini, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Akizungumza katika kumbukumbu hiyo, Abbas Akhundi, Waziri wa Uchukuzu wa Iran ameashiria mafanikio ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia na kundi la 5+1 na pia kuondolewa vikwazo na kusema, ushindi wa Iran katika kadhia ya nyuklia si tishio kwa nchi yoyote.

Ikumbukwe kuwa miaka 37 iliyopita siku kama ya leo, yaani tarehe Mosi Februari mwaka 1979, Imam Ruhullah Khomeini (MA) mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alirejea nchini na kupokewa kwa shangwe kubwa na wananchi baada ya kuishi uhamishoni kwa kipindi cha miaka 15. Chanzo irib