Monday, February 1, 2016

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi -Sehemu ya Pili

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiAssalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi na karibuni kuwa nasi katika mfululizo huu wa vipindi maalumu vinavyokujieni kwa mnasaba wa maadhimisho ya Alfajiri Kumi ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambapo leo tutayazungumzia Mapinduzi ya Kiislamu, kama kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi. Endeleeni kuwa nami hadi mwisho wa kipindi kusikiliza niliyokuandalieni katika mfululizo huu.

Amma taathira ya tatu ya Mapinduzi ya Kiislamu imetokana na kulinda thamani na tunu za Kiislamu. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kinyume na mapinduzi mengi yaliyotokea duniani, hayakukengeuka njia yake ya asili, na hayakuwa tayari kwa hali yoyote ile kuachana na thamani zake aali na malengo yake matukufu licha ya vizuizi na mashinikizo ya kila namna yaliyokabiliana nayo. 

Kwa sababu hiyo, Mapinduzi ya Kiislamu yamekuwa ni nembo ya harakati ya kupigania haki katika uga wa maisha ya kisiasa na kijamii.

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiMUZIKI
Mapinduzi ya wananchi wa Iran yalikuwa na mvuto mkubwa kwa mataifa mengine katika sura tofauti; na kutokana na kuwa tajiriba moja mpya iliyotokana na thamani za kidini na kiutu yalitoa ilhamu kwa harakati na mabadiliko ya ulimwengu na kwa mageuzi ya kijamii.

Kabla ya kujiri Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kwa kuzingatia kutawala duniani fikra mbili za Ubepari na Ukomunisti ilijengwa dhana kwamba mifumo ya tawala haingeweza kutoka nje ya mduara wa moja ya mifumo miwili ya Demokrasia ya Kiliberali na Usoshalisti; na kwa hivyo kama yangetokea mapinduzi yoyote yale duniani yangekuwa hayana budi kuegemea kwenye mhimili wa moja ya fikra mbili hizo na kutegemea msaada na uungaji mkono wa moja kati ya kambi mbili kuu za Mashariki na Magharibi. 

Kwa mintaarafu ya hayo wana nadharia wengi wa Mapinduzi walitaka kuyahakiki Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika kalibu ya moja ya fikra mbili hizo, katika hali ambayo vuguvugu la mapinduzi hayo hadi ushindi wake, pamoja na harakati yake na malengo yake vimejipambanua kikamilifu na fikra hizo.

Ukweli ni kwamba thamani na umuhimu wa mapinduzi yoyote vinategemea ghaya na malengo makuu yanayofuatiliwa na mapinduzi hayo. Ukubwa na udogo wa malengo hayo huwa unachangia kwa kiwango kikubwa gharama ambazo kila mapinduzi yanalazimika kuzilipia. Kadiri malengo ya mapinduzi yanapokuwa na utukufu na mvuto mkubwa zaidi ndivyo yanavyolazimika kuhimili na kuvumilia tabu, misukosuko na mashinikizo makubwa zaidi ili kuweza kuyafikia malengo hayo.

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiMashinikizo na misukosuko ambayo Mapinduzi na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu umeihimili na kuivumilia katika muda wa miaka 38 iliyopita ni ithbati na ushahidi wa kuthibitisha ukweli huu, kwamba ili kufikia ghaya na malengo yake matukufu, taifa la Iran limesimama imara kukabiliana na mashinikizo yote; na kigezo cha kusimama imara huko ni kukataa ubeberu wa madola makubwa duniani na mfumo uliojengwa kwa msingi wa ubabe na utumiaji mabavu, udhalilishaji watu na ubaguzi wa rangi. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalidhihiri na kuasisi mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kwa madhumuni ya kufikia malengo hayo.

MUZIKI
Historia ya Mapinduzi ya Kiislamu inaonyesha kwa uwazi kabisa sababu kuu ya uadui wote huu na njama zote hizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwemo Vita vya kulazimishwa na vikwazo vya uchumi; nayo ni hofu ya taathira za mapinduzi hayo na kuwa kigezo cha kuigwa na wananchi wa mataifa mengine.

Uistikbari wa dunia ambao ulihisi umepoteza maslahi na manufaa yake ya kimaada kutokana na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ulianzisha fitna na njama mara baada ya ushindi wa mapinduzi hayo kwa dhana kwamba utaweza kuyasimamisha, kuyapotosha muelekeo wake na hatimaye kuyasambaratisha. Na ndiyo maana uliamua kukabiliaana na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu; lakini haukupata tija nyengine ghairi ya kushindwa na kugonga mwamba.

Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za MagharibiMhimili mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni nafasi na mchango wa wananchi. Wananchi wa Iran waliendesha mapambano ya muda mrefu na kuweza kuusambaratisha utawala kibaraka wa Kifalme na kuasisi Mfumo wa Kiislamu. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameweza baada ya miaka mingi kuuondoa Uislamu na jamii za Kiislamu kwenye hali ya kutengwa. 

Yakiwa mithili ya injini isukumayo merikebu, yametoa msukumo wa mwamko kwa harakati za Kiislamu na uelewa kwa wananchi wa mataifa ya Kiislamu ya eneo wa kutambua haki zao na uwezo walionao. Kwa hivyo tunaweza kusema kuwa fikra za kisiasa za Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimetokana na msingi wa mapambano katika njia ya kutetea haki na uadilifu. 

Ni kwa sababu hiyo, ndiyo maana Uistikbari wa dunia ukiongozwa na Marekani uliamua tokea awali kulipa kipaumbele cha kwanza katika sera zake suala la kukabiliana na Mapinduzi ya Kiislamu ili kwa mawazo yake uuangushe Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Katika muda wote wa miaka 38 iliyopita, Marekani imekuwa ikichukua kwa sura ya mtawalia hatua za kiadui na kihasama dhidi ya taifa la Iran. Lakini muqawama wa taifa hili na kusimama kwake imara kumetoa somo na funzo kubwa kwa maadui zake.

Harakati hii adhimu iliyoandamana na muqawama na kusimama imara kuyakabili mashinikizo imesababisha kujiri mageuzi makubwa katika mahusiano ya Iran na ulimwengu wa nje. Ni kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu 
 Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kwamba kukithiri kwa vitisho ni ishara ya kuwa na nguvu Mfumo wa Kiislamu; kwa sababu kama Jamhuri ya Kiislamu ingekuwa haina nguvu na ushawishi wenye taathira, wasiolitakia mema taifa la Iran wasingehaha na kuchacharika kiasi hiki katika kupanga na kutekeleza kila aina ya njama dhidi ya taifa hili.

Wasikilizaji wapenzi kipindi chetu hiki maalumu cha Alfajiri Kumi kimefikia tamati. Ni matumaini yangu kuwa mumenufaika na yale mliyoyasikia katika kipindi hiki. Msiache kujiunga nasi tena katika mfululizo ujao wa vipindi hivi. 

Nakuageni basi huku nikikutakieni usikilizaji mzuri wa sehemu iliyosalia ya matangazo yetu

No comments: