Assalaamu Alaykum wasikilizaji wapenzi na karibuni kuwa nasi katika
mfululizo huu wa vipindi maalumu vinavyokujieni kwa mnasaba wa
maadhimisho ya Alfajiri Kumi ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya
Iran, ambapo leo tutayazungumzia Mapinduzi ya Kiislamu, kama kigezo cha
kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi. Endeleeni
kuwa nami hadi mwisho wa kipindi kusikiliza niliyokuandalieni katika
mfululizo huu.
MUZIKI
Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ni moja ya matukio makubwa zaidi ya karne ya 20; na likiwa moja ya matukio yasiyo na mfano wake katika zama hizi yalifungua ukurasa mpya katika historia ya mwanadamu na kuwa chemchemi ya mabadiliko makubwa katika nyuga za kiutamaduni, kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Mapinduzi ya
Kiislamu kwa wananchi wa Iran lilikuwa ni hitajio na jambo la lazima,
ambalo liligeuka kuwa mwanzo wa harakati mpya katika uga wa muqawama wa
mataifa, katika kukabiliana na mifumo na tawala za kibeberu. Na ndiyo
maana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulikuwa ni tukio ambalo mwangwi
wake ulivuka mpaka wa kieneo.
Kimsingi, kila Mapinduzi yanayojiri katika eneo la kijiografia la watu huwa na athari na kusababisha mageuzi na mabadiliko ya msingi; lakini kitu kinachoyalinda mapinduzi hayo na kuyafanya yadumu ni upana na ukubwa wa taathira zake.
Sifa hii
imeonekana kwa uwazi kabisa na kwa kiwango kikubwa katika Mapinduzi ya
Kiislamu ya Iran; kiasi kwamba mataifa mengi ya wanyonge duniani
yalihisi kuwa yataweza kupata matamanio na matarajio yao kwa kufuata
kigezo cha Mapinduzi ya Kiislamu.
Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
ulivuruga mlingano uliokuwa ukitawala katika mfumo wa kisiasa wa kieneo
na kimataifa; na kwa kutegemea msingi wa "nguvu ya wananchi" na
"kupigania kujitawala" ukafanikiwa kuonyesha mfano wa kukabiliana na
siasa za kibeberu.
Kwa msingi huo, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
nchini Iran ulizingatiwa na kupewa umuhimu kutokana na kuwa chemchemi ya
kutoa ilhamu kwa mataifa yanayopigania uhuru na kujitawala duniani; na
hadi leo hii pia licha ya kupita karibu miongo minne, yangali yanatoa
ilhamu kwa harakati za kimapinduzi katika nchi mbalimbali.
Kwa mtazamo wa wana nadharia wa Mapinduzi yaliyojiri duniani, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yana taathira tatu muhimu na za kudumu; na ndiyo sababu iliyoyafanya madola ya kiistikbari yachacharike na kuhaha kwa ajili ya kukabiliana na mapinduzi hayo.
Taathira ya kwanza na muhimu zaidi ya
ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ilikuwa ni kutoa changamoto kwa
mfumo wa Ubeberu duniani. Kwa ushindi wake wenye lengo maalumu,
mapinduzi haya yalionyesha kuwa hata kama taifa litakuwa mikono mitupu
bila ya kuwa na silaha yoyote, linao uwezo wa kuwa chachu ya kuleta
mabadiliko makubwa hata katika mlingano na mahesabu ya madola makubwa
duniani.
Taathira ya pili ni kwamba Mapinduzi ya Kiislamu yalionyesha
nguvu na uwezo halisi wa taifa la watu bila ya kutegemea msaada na
uungaji mkono wa lolote kati ya madola makuu ya dunia wakati huo. Na
hiyo ndiyo sababu iliyoyafanya Mapinduzi ya Kiislamu yawe ni msukumo wa
kujiri mageuzi makubwa ya kisiasa katika upeo wa ulimwengu mzima.
Mageuzi na mabadiliko hayo yaliwaonyesha walimwengu nguvu kubwa na uwezo
wa kisiasa wa dini ya Uislamu na kuhuisha harakati adhimu ya kujikomboa
na ubeberu na kusimama imara kukabiliana na ukoloni.
No comments:
Post a Comment