Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu ya
Iran amesema, umoja wa taifa la Iran ndio sababu ya ushindi wa Mapinduzi
ya Kiislamu na kuangushwa utawala wa kifalme wa Pahlavi.
Ayatullah Ali Akbar Hashemi Rafsanjani ameyasema hayo katika sherehe
za kukumbuka siku aliporejea nchini Iran Imam Khomeini MA katika uwanja
wa ndege wa Mehrabad mjini Tehran. Ameongeza kuwa aghalabu ya watu wa
Iran walitaka Mapinduzi ya Kiislamu na kwa umoja wao waliweza kuuangusha
utawala wa Shah Pahlavi.
Ayatullah Rafsanjani ameendelea kusema kuwa, taifa la Iran linapaswa
kuendeleza harakati za kufikia malengo matukufu ya Imam Khomeini,
mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumza katika kumbukumbu hiyo, Abbas Akhundi, Waziri wa Uchukuzu
wa Iran ameashiria mafanikio ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia na
kundi la 5+1 na pia kuondolewa vikwazo na kusema, ushindi wa Iran katika
kadhia ya nyuklia si tishio kwa nchi yoyote.
Ikumbukwe kuwa miaka 37 iliyopita siku kama ya leo, yaani tarehe Mosi
Februari mwaka 1979, Imam Ruhullah Khomeini (MA) mwasisi wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran, alirejea nchini na kupokewa kwa shangwe kubwa na
wananchi baada ya kuishi uhamishoni kwa kipindi cha miaka 15. Chanzo irib
No comments:
Post a Comment