Friday, November 6, 2015

Jeshi la Yemen latungua ndege ya Saudi Arabia

Habari kutoka Yemen zinasema kuwa ndege ya kivita ya Saudi Arabia imetunguliwa na jeshi la Yemen katika mkoa wa Sana’a.

Duru za habari zimeripoti kuwa, ndege hiyo ya Saudia imetunguliwa mapema leo na kikosi cha anga cha jeshi la Yemen katika mji wa Bilad al-Rus, magharibi mwa mkoa wa Sana’a. Habari zaidi zinasema kuwa rubani wa ndege hiyo ya Aal-Saud anazuiliwa na jeshi la Yemen.

Jeshi la anga la Yemen limekuwa likiangusha ndege pamoja na drone za Saudia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo katika kipindi cha miezi michache iliyopita. Siku chache zilizopita, Wapiganaji wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen na waitifaki wao waliua makumi ya wanajeshi wa Saudi Arabia katika mashambulizi ya kulipiza kisasi katika mkoa wa Ta'izz, 
 
kusini magharibi mwa Yemen. Saudi Arabia na waitifaki wake tarehe 26 Machi mwaka huu walianzisha mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen wasio na hatia kwa kisingizio cha kuirejesha madarakani serikali ya Yemen iliyojiuzulu. 
 
Mashambulizi hayo mbali na kuharibu miundombinu, hospitali, misikiti, shule na nyumba za raia, yameua na kujeruhi pia maelfu ya watu. Karibu Wayemen 7,100 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, wameuawa katika mashambulizi hayo ya kinyama ya Saudia. Chanzo Irib

Jeshi la Niger lashambulia maeneo ya Boko Haram

Kwa mara ya kwanza jeshi la Niger limefanya mashambulizi yake ya anga dhidi ya maeneo ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.
Jeshi la Niger limeyashambulia maeneo ya kusini mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamekuwa yakitumiwa na wanachama wa kundi hilo katika kuendeleza jinai za kigaidi. Hata hivyo hadi sasa jeshi hilo bado halijatoa taarifa kamili kuhusiana na operesheni hizo, ingawa gavana mpya wa eneo la Diffa, kusini mashariki mwa Niger, amethibitisha kutumiwa silaha za jeshi la anga katika mashambulizi hayo.
Katika mashambulizi hayo jeshi la Niger limeshambulizi maeneo ya Boko Haram karibu na kijiji cha Dagaya katika eneo hilo la kusini mashariki mwa nchi hiyo. Hivi karibuni serikali ya Niamey ilitangaza hali ya hatari katika eneo la Diffa, liliko katika mpaka wa pamoja na Nigeria.
Jeshi la Niger lilijiunga na operesheni ya majeshi ya nchi za Chad, Nigeria na Cameroon dhidi ya wanachama wa kundi hilo la kitakfiri la Boko Haram, mwanzoni mwa mwaka huu wa 2015, operesheni zinazotajwa kuwa na mafanikio makubwa.Chanzo Irib