Habari kutoka Yemen zinasema kuwa ndege ya kivita ya Saudi Arabia imetunguliwa na jeshi la Yemen katika mkoa wa Sana’a.
Duru za habari zimeripoti kuwa, ndege hiyo ya Saudia imetunguliwa
mapema leo na kikosi cha anga cha jeshi la Yemen katika mji wa Bilad
al-Rus, magharibi mwa mkoa wa Sana’a. Habari zaidi zinasema kuwa rubani
wa ndege hiyo ya Aal-Saud anazuiliwa na jeshi la Yemen.
Jeshi la anga la Yemen limekuwa likiangusha ndege pamoja na drone za
Saudia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo katika kipindi cha miezi
michache iliyopita. Siku chache zilizopita, Wapiganaji wa harakati ya
Ansarullah nchini Yemen na waitifaki wao waliua makumi ya wanajeshi wa
Saudi Arabia katika mashambulizi ya kulipiza kisasi katika mkoa wa
Ta'izz,
kusini magharibi mwa Yemen. Saudi Arabia na waitifaki wake
tarehe 26 Machi mwaka huu walianzisha mashambulizi dhidi ya wananchi wa
Yemen wasio na hatia kwa kisingizio cha kuirejesha madarakani serikali
ya Yemen iliyojiuzulu.
Mashambulizi hayo mbali na kuharibu miundombinu,
hospitali, misikiti, shule na nyumba za raia, yameua na kujeruhi pia
maelfu ya watu. Karibu Wayemen 7,100 wengi wao wakiwa ni wanawake na
watoto, wameuawa katika mashambulizi hayo ya kinyama ya Saudia. Chanzo Irib
No comments:
Post a Comment