Kwa mara ya kwanza jeshi la Niger limefanya mashambulizi yake ya
anga dhidi ya maeneo ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.
Jeshi la Niger limeyashambulia maeneo ya kusini mashariki mwa nchi
hiyo ambayo yamekuwa yakitumiwa na wanachama wa kundi hilo katika
kuendeleza jinai za kigaidi. Hata hivyo hadi sasa jeshi hilo bado
halijatoa taarifa kamili kuhusiana na operesheni hizo, ingawa gavana
mpya wa eneo la Diffa, kusini mashariki mwa Niger, amethibitisha
kutumiwa silaha za jeshi la anga katika mashambulizi hayo.
Katika mashambulizi hayo jeshi la Niger limeshambulizi maeneo ya Boko
Haram karibu na kijiji cha Dagaya katika eneo hilo la kusini mashariki
mwa nchi hiyo. Hivi karibuni serikali ya Niamey ilitangaza hali ya
hatari katika eneo la Diffa, liliko katika mpaka wa pamoja na Nigeria.
Jeshi la Niger lilijiunga na operesheni ya majeshi ya nchi za Chad,
Nigeria na Cameroon dhidi ya wanachama wa kundi hilo la kitakfiri la
Boko Haram, mwanzoni mwa mwaka huu wa 2015, operesheni zinazotajwa kuwa
na mafanikio makubwa.Chanzo Irib
No comments:
Post a Comment