|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana
na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi
Agosti 1, 2015 mara baada ya kurejea kutoka Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove.
|
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015
akitokea Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove. |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine
waliofika kumpokea alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015
akitokea Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove.
|
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa
mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani Madabida alipowasili katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa
Jumamosi Agosti 1, 2015 akitokea Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove. | |
PICHA NA IKULU
……………………
Akiwa nchini Australia Rais
Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Australia,
Bwana Tony Abbot ambaye alimpongeza kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa
kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba nchini Tanzania.
Rais Kikwete pia alikutana na
kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa
Peter Cosgrove, kabla ya kukutana na wawekezaji wakubwa wa Australia
ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania ambapo walizungumzia namna ya
kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inavyoweza
kunufaika kutokana na kupata gesi.
Tayari Serikali ya Australia na
makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika
vyuo vya ufundi stadi VETA na tafiti mbalimbali katika Kilimo.
Rais Kikwete alihitimisha ziara
yake kwa kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo
Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa
kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa
ujumla.