Baada jana TFF kutoa maamuzi
kuhusu utata uliojitokeza kwenye mkataba kati ya klabu ya Simba na
Ramadhani Singano ‘Messi’, leo mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba
Zacharia Hans Poppe amesika kwenye kituo kimoja cha redio cha jijini
Dar es Salaam akizungumzia sakata hilo huku akihoji ni nani aliye
mwambia Singano yupo huru?
Poppe amesema kikao
kilichofanyika jana na kuongozwa na katibu mkuu wa TFF Selestine
Mwesigwa hakikuwa na mamlaka wala madhumuni ya kuamua upi ni mkataba
halali kati ya mkataba alionao Messi au mkataba uliopo Simba. Badala
yake kilikuwa ni kikao cha kutafuta suluhu ili mambo yaweze kwenda sawa
kati ya pande hizo mbili.
“Kikao kilichofanyika jana
hakikufanyika kwa madhumuni ya kuamua nani kashinda na nani kashindwa,
hakikuwa na ‘mandate’ hayo, hakina maamuzi ya kusema mkataba huu ni
halali na huu sio halali. Katibu mkuu wa TFF amesema wazi kilichofanyika
jana ni ‘mediation’, pale hapakuwa na maamuzi ya kuchambua mkataba upi
upo ‘right’ wala hawakufikia hatua hiyo”, amesema Poppe.
“Ila walichokisema pale ni
kwamba, kabla hatujafika kwenye kamati ya sheria na hadhi za wachezaji
ambako pale ni mashtaka sasa na hukumu, hivi hili suala halizungumziki?
Ndio kitu kilichofanyika jana na kilitokana na yeye mwenyewe ‘Messi’
kuulizwa, wewe ulivyozua hili varangati Simba ulikuwa unataka nini,
kuondoka Simba? Akasema hapana mimi nataka kuendelea kuchezea Simba.
Akaulizwa mwakilishi wetu Collins akasema mbona sisi na mkataba tumesha
mpatia?”, aliongeza.
“Ndio wakasema kama suala liko
hivi linazungumzika, kwanini lisiende kwenye mkopndo huo. Kumbuka mwanzo
mimi nilieleza kuwa, huyu mchezaji wakati amekuja kuhoji kuhusu mkataba
wake na kuona kwamba yeye anazungumzia mkataba wake umeisha na sisi
tunasema haujaisha, tulimweleza kwamba hili suala linazungumzika vizuri
tu, kama wewe huutaki huu mkataba njoo tukae tukupe mkataba mpya lakini
mkataba wako ni huu sasa yeye akaendelea kung’ang’ania na sisi tunaona
hili suala ni bora lifike mwisho wake”, amesema.
“Kama hatutaelewana hakuna
mkataba mpya mezani tunarudi kwenye mkataba wetu ulipo kwamba sisi
mkataba wetu unamalizika 2016, sasa ndio tutakwenda kwenye kamati ya
sheria na hadhi za wachezaji hao ndio watakaotoa uamuzi sasa mkataba upi
ni halali”, amefafanua.
“Baada ya kutoka kwenye kikao cha
jana, Messi kaenda kuzunmgumza kwamba yeye yuko huru sasahivi,
aliyemwambia yuko huru nani? Mwesigwa kaulizwa pale kama mchezaji yupo
huru kasema hapana, na haikutakiwa kuzungumza, mtu aliyetakiwa
kuzungumza pale alikuwa ni katibu peke yake”, alisisitiza.
Chanzo:Shafihdauda.co
No comments:
Post a Comment