RAIS Jakaya Kikwete ambaye amekuwa katika
ziara za kuaga washirika wa mandeleo katika nchi za Scandinavia,
amekataliwa kuingia Denmark kwa madai kuwa ziara yake itatumika kisiasa
kumnufaisha Waziri Mkuu wa sasa wa Denmark.
Nchi hiyo inatarajia kufanya
uchaguzi wake mkuu wiki ijayo. Zuio hilo limekuja baada ya vyombo vya
habari na vyama vya siasa kudai kuwa ziara hiyo ingetumika kumnufaisha
Waziri Mkuu aliyepo kwa kumpa muda wa ziada mbele ya vyombo hivyo wakati
huu wa kampeini.
Vyama vyote vya kisiasa vinapata muda
sawa mbele ya vyombo vya habari na kwa hiyo uwepo wa Rais Kikwete nchini
Denmark ungesababsha Waziri Mkuu aliyepo madarani kuonekana mara nyingi
akimpokea mgeni wake.
Rais Kikwete hivi karibuni amefanya ziara
katika nchi za Finland, Sweden, Uholanzi ikiwa ni sehemu ya kuaga
kutokana na muda wake wa kuwa madarakani kufikia ukingoni.
Chanzo:Mwanahalisi
No comments:
Post a Comment