Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amemsifu sana mkewe Hillary na kusema anafaa kuongoza taifa hilo.
Ameambia
kongamano kuu la chama cha Democratic mjini Philadelphia kwamba mkewe
ndiye “mfumaji bora zaidi niliyewahi kukutana naye”.
Kwenye hotuba
yenye hisia kali, amemweleza Hillary kama “rafiki mkubwa” na akasimulia
walivyokutana na jinsi anavyojitolea katika utumishi wa umma.
Saa chache awali, mkewe aliibuka kuwa mwanamke wa kwanza nchini Marekani kuidhinishwa kuwania urais na chama kikubwa
Bi
Clinton alihitimisha shughuli za usiku huo wa Jumanne kwa ujumbe wa
video ambapo alisema: “Siamini kwamba tumefanikiwa kuweka ufa mkubwa
zaidi katika dari hili la kioo”, akirejelea hotuba ya mkewe Rais Barack
Obama, Michelle, siku ya kwanza ya kongamano.
“Na iwapo kuna
wasichana wadogo huko ambao hawajalala na wananitazama, ningependa
kuwaambia, huenda nikawa rais wa kwanza mwanamke Marekani na mmoja wenu
anaweza kunifuata.”
Awali, Bi Clinton alisimulia walivyokutana katika Chuo cha Uanasheria Yale mwaka 1971.chanzo:bbc