Tuesday, May 26, 2020

“Mzalendo ni Mtu ambae siku zote mtazamo wake ni hapa Kazi tu” Sheikh Jalala

Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akionyesha ishara ya Matumizi ya Akili, na kusema kuwa Ugonjwa wa Corona ileleta Uhuru wa Kufikiri, juzi masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Ugonjwa wa Covid 19 umeleta Uhuru kwa bara la Afrika ikiwemo Tanzania kwa kuanza tafiti za Kutafuta dawa na ishara za Uzalendo na badala ya kutomsubiria Shirika la Dawa Duniani.

“Uhuru wa Kufikiria imeletwa na Balaa hili la Ugonjwa wa Corona, Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wamepata dawa, haya ni maendeleo makubwa hawa ni watafiti wetu wa ndani ya nchi, nah ii ndio dalili ya Uzalendo, mzalendo ni Yule ambae hataki kunyanyua mikono akaomba omba, mzalendo ni Yule ambae mtizamo wake siku zote ni hapa kazi tu, hakuna kuomba omba watu” Sheikh Jalala amesema.

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (TIC) Sheikh Abdallah Seif akiongoza Swala ya Eid al Fitiri, Juzi Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Sheikh Jalala amesema hayo wakati akiongea na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Khutba ya Swala ya Eid al Fitiri, iliyoswaliwa Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

“Jumuiya ya Afrika Mashiriki Viongozi wake wanawasiliana mara kwa mara kuzungumza ni namna gani tutatatua tatizo hili la Ugonjwa wa Corona, mtazamo huu wa waafrika wenyewe na uhuru wa kuangalia wenyewe na maraisi wetu, mtazamo huu kwa kuufanya wao wenyewe ni na uhakika afrika itaondoka na balaa la Umasikini, balaa la Omba omba na balaa na Ubungufu wa Bajeti zao” Sheikh Jalala amesema.

" Tutakuwa sisi ni wachache wa Fadhila, tutakuwa sisi hatujatenda haki kwamba kwa Uhuru wa Fikra na Mtizamo kama hatukumtaja Kiongozi wa nchi yetu Mhe. John Pombe Magufuli, kwa mtizamo wake na uzalendo aliokuwa nao lakini na msimamo ambao leo dunia inauzungumza kwamba ni msimamo wa Kishujaa na ni msimamo wa Kiume katika Vita dhidi ya Ugonjwa wa Corona" Sheikh Jalala amesema.




.”Masjid al Aqswa ndio Chimbuko ya Amani Duniani” Sheikh Jalala

Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Kilele cha Siku ya Kimataifa ya Quds, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds na Masjid al Aqswa ndio chimbuko la Amani, na Usalama wa Dunia na kuitaka Watanzania kuwa wamoja katika kuhakikisha Palestina na nchi zinginezo wanapata Amani.

“Masjid al Aqswa , Quds au Palestina au tukio la Aqswa ni tukio pekee ambalo linaweza kutengeneza Umoja kati ya Waislam, Wakristo na Mayahudi na ndio chimbuko la kuweza Kuleta Amani duniani” Sheikh Jalala amesema.


Maulana Sheikh Jalala amesema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika Kilele cha Siku ya Kimatifa ya Quds,Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

Masjid al Aqswa ulioko Palestina katika mji wa Jerusalemu ndio Qibla cha Kwanza cha Waislam na ni jambo linalowahusu Waislamu na ndio kiini cha kuwakusanya Waislamu , Sheikh Jalala amesema.

Masjid al Aqswa, Siku ya Quds inaweza kuwa Kiunganishi cha Waislamu, Wakristo pamoja na Mayahudi na wakapa suluhisho la matatizo yanayowakabili, Tanzania ni nchi ya Amani, watu wake hawajui Kubaguana.

“Siku ya Quds huwa Inakumbukwa na Waislam,wapenda Amani na wanaojali Utu”Sheikh Jalala

Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika Semina ya Maimam kuelekea  Siku ya Kimataifa ya Quds, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislam, Wakristo, Mayahudi na Watanzania kuwa kitu kimoja katika kuipigania Mashariki ya Kati ikiwepo Palestina na sehemu zinginezo kuwa katika Amani na Salama.

“Siku hii ya leo (Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani) ndugu zangu Waislam na wasiokuwa Waislamu kama tunavyokumbuka Qibla cha Kwanza vilevile tunakumbuka ardhi ya Mashariki ya kati ikiwemo na Palestina ni ardhi iliyobarikiwa , ni ardhi yenye Baraka, kwanini ni ardhi yenye Baraka? Ni kwa sababu Mitume tunaowatambua sisi wametokea pale mashariki ya Kati, ni sehemu inayotuhusu, ni sehemu inayowahusu Waislamu, Wakristo na Mayahudi” Sheikh Jalala amesema

Sheikh Jalala amesema hayo katika Semina ya Maimam na Masheikh baadhi wa Mkoa wa Dar es salaam katika kukumbuka Siku ya Kimataifa ya Quds, ambayo huwa kilele chake huwa siku ya Ijumaa ya Mwisho katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.


“Sisi tunambue yakwamba kama waislam kumbe Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) anatokea sehemu moja,kwahiyo sote waislam ni kitu Kimoja, kama nabii Issa/ Yesu Kristo (a.s) kwa ndugu zetu wakristo wao ndio Kiongozi wao, Nabii Mussa / Mosses (a.s) ndugu zetu Mayahudi ndio Kiongozi wao, hawa wote wanatokea Mashariki ya kati, hii inamaana Quds au Palestina inaweza kutukusanya watu wote wa dini tatu tukawa kitu kimoja”.Sheikh Jalala amesema.

“Sisi hapa Tanzania tunajulikana ni Kisiwa cha Amani, Watanzania tunajulikana ni watu hatubaguani kwa dini zetu tunaishi kama watanzania, lakini ndugu zangu hili la Amani halipo katika ardhi ya Palestina, halipo Libiya, halipo Syria halipo sehemu zinginezo ni wajibu wetu kuyakumbuka ya wenzetu, kuwaombea Mungu na kutaka yatatuke ili na wao wabakie katika salama na Amani kama tulivyobakia sisi” Sheikh Jalala amesema.