Tuesday, May 26, 2020

.”Masjid al Aqswa ndio Chimbuko ya Amani Duniani” Sheikh Jalala

Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Waandishi wa Habari katika siku ya Kilele cha Siku ya Kimataifa ya Quds, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds na Masjid al Aqswa ndio chimbuko la Amani, na Usalama wa Dunia na kuitaka Watanzania kuwa wamoja katika kuhakikisha Palestina na nchi zinginezo wanapata Amani.

“Masjid al Aqswa , Quds au Palestina au tukio la Aqswa ni tukio pekee ambalo linaweza kutengeneza Umoja kati ya Waislam, Wakristo na Mayahudi na ndio chimbuko la kuweza Kuleta Amani duniani” Sheikh Jalala amesema.


Maulana Sheikh Jalala amesema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika Kilele cha Siku ya Kimatifa ya Quds,Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

Masjid al Aqswa ulioko Palestina katika mji wa Jerusalemu ndio Qibla cha Kwanza cha Waislam na ni jambo linalowahusu Waislamu na ndio kiini cha kuwakusanya Waislamu , Sheikh Jalala amesema.

Masjid al Aqswa, Siku ya Quds inaweza kuwa Kiunganishi cha Waislamu, Wakristo pamoja na Mayahudi na wakapa suluhisho la matatizo yanayowakabili, Tanzania ni nchi ya Amani, watu wake hawajui Kubaguana.

No comments: