Makamu wa Rais Mstaafu Dk. Bilal alisema hayo jana jijini Dar es Salaam
katika kuadhimisha siku ya usonji duniani iliyoandaliwa na Taasisi ya
'KSIJ Central Board of Education' katika shule ya Al-Muntazir ambapo
ameipongeza taasisi hiyo kwa kuanzisha kitengo maalum kinachotoa mafunzo
kwa watoto wenye usonji na kufafanua kuwa siyo kazi rahisi kwani
inahitaji rasilimali watu.
wataalamu, fedha kuwa na moyo na uthubutu
hivyo wadau na serikali kwa pamoja waunge mkono jitihada hizo na
atafikisha kilio hicho kwa serikali ili kuunga mkono jinsi ya kuwasaidia
watoto hao.
Matembezi
hayo yalikuwa na kauli mbiu inayosema kuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE” ikiwa na
maana ya kuwapenda na kuwapatia ulinzi watoto wenye mahitaji maalumu.
Dkt
bilal aliongeza kuwa kwa kutambua athari za ugonjwa huo wa asonji ipo
haja kwa jamii kujitoa kwa hali na mali hili kuwafanya na wao kujisikia
kuwa ni sehemu ya jamii kwa kuwapatia misaada mbalimbali.
Mgeni Rasmi Dr. Bilal aliweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja
taslimu alizo zitoa hapo akimkabidhi Mwenyekiti wa Khoja Shia Itha ashel Jamaat
central board of education Mr Intiaz Lalji kwa kuweza kuongeza nguvu katika
zoezi la kuwasaidia vijana hao. Huku akiwasilisha mchango Makamu wa Raisi wa
sasa Mama Samia suluhu aliyeweza kutoa mchango wa million 5.
Imtiaz Lalji Mwenyekiti wa KISJ Central Board of Education akiongea mbele ya hadhira kwenye Maadhimisho ya Watu wenye Usonji Duniani katika Shule ya Al-Muntazir Boy, Dar es salaam. |
Kwa upande wake Mwenyejkiti
wa Taasisi ya KSIJ Center of education bwana Imtiaz Lalji alitoa wito
kwa jamii kuwa karibu na watu wenye ugonjwa wa usonji sambamba na
kuwasaidia kuwawezesha kutimiza ndoto zao.
Alisema
kupitia taasisi ya KSIJ Center of education tayali wameshatoa mafunzo
kwa wanafunzi watatu wenye usonji na mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo
wamewaajilikama walimu wasaidizi shuleni hapo hivyo kutoa wito serikali
pamoja na taasisi zisizo za kiserikali kuanza kutoa nafasi za ajila kwa
watu hao.