Amani ya Mwenyezi Mungu iwe kwenu
Nyote.
Siku hii ya leo ambayo kwa tarekh ya Kiislamu tunaita ni
Mwezi 9,ni siku ambayo wanazuoni wa Kiislamu wameitangaza kuwa ni Siku ya
Mwanamke wa Kiislamu Duniani, sababu kubwa ya Tangazo hilo nikutokana na
kuzaliwa Bint ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambae Bint huyu na Mama huyu na dada
huyu ananafasi kubwa katika Dini ya Uislamu.
Mama huyu ambae tunakumbuka mazazi yake ambae Maulamaa
wameitangaza kuwa ni siku ya Mwanamke wa Kiislamu Duniani daraja lake mama huyu
katika Uislamu ni kama vile daraja la Maryam bint Imran, Mama yake Nabii Issa
(a.s). Lakini kwanini kukumbukwa mama huyu lakini vilevile kwani kutangzwa ni
siku ya Mwanake wa Kiislamu Duniani.
Sababu kubwa ni daraja
la mwanamke na nafasi ya mwanamke katika jamii na katika Uislamu.Uislamu
unamuangalia Mwanamke katika mambo yafuatayo, kwanza Uislamu unamuangalia
Mwanamke kwamba ni mwanadamu wa Kawaida kama vile Mwanamume.kwa ibara nyingine
nzuri Uislamu hautofautishi kati ya jinsia ya Kiume na jinsia ya Kike.
Na tunaamini kakika Uislamu ya kwamba jinsia hizi mbili zote
zipo sawasawa, jinsia ya Kike na Jinsia ya Kiume. Kwahiyo siku ya Mwanamke wa
Kiislamu Duniani ni siku ya kufuta maneno yanayowezwa kusemwa ya kwamba
mwanamume ni bora kuliko mwanamke, hapana ni jinsia mbili ambazo zipo sawasawa
kama ni mapungufu basi yapo kwa wanaume na yapo vilevile kwa wanawake.
Jambo la pili ni jambo la haki, mwanamume anahaki kwenye
mambo mengi na mambo kadhaa haki hizo vilevile zipo kwa mwanamke, kwa mfano
mwanamke anayohaki ya kufanya kazi? Je katika Uislamu mwanamke anayohaki ya kufanya kazi? Jawabu ndio. Haki hiyo
vilevile anayo mwanamke katika Uislamu.
Mwanamume anayohaki ya kuendesha gari, Je mwanamke
anaruhusiwa kuendesha gari? Ndio mwanamke vilevile anayohaki ya kuendesha gari
katika uislamu. Mwanamume anayohaki ya Elimu, mwanamume anayohaki ya Kusoma
mpaka kufikia ngazi za juu, je haki hiyo mwanamke anayo katika uislamu? Ndio
mwanamke vilevile anayohaki ya kusoma na kusomeshwa mpaka ngazi za juu.
Katika siku hii ya kumkumbuka mwanamke duniani, katika sikun
hii ya kumkumbuka mwanamke wa Kiislamu Duniani moja ya jambo la kuliangazia ni
jambo la Elimu ya kwamba wazazi watambue kama walivyokuwa na haki kumsomesha
kijana wa kiume na mototo wa kiume vilevile ni haki yao kumsomesha binti wa
kike na kijana wa kike na kumsomesha hakuna kiziwizi maalumu ikiwa na maana
asomeshwa mpaka ngazi Fulani kasha basi.
Kulikuwa na fikra ambazo zinapatikana kwenye baadhi ya
maandiko ambayo maandiko hayo tunayasema ni maandiko ya Kimakosa kwa mfano kuna
baadhi ya fikra zinaona Mwanamke ndie aliefanya makosa alipokuwa kule Peponi na
ikawa ndio sababu ya kufukuzwa adam na hawa kwamba sababu ilikuwa ni mwanamke.
Hapana dini ya Uislamu
inaangalia yakwamba makosa yaliyofanya ndani ya pepo hayana mahusiano na Mwanamke
na kwamba mwanamke ni kiumbe kama vile viumbe wengine wa kawaida. Mwanamume
anayokarama anayoheshima, je heshima hii ipo kwa mwanamke?
Mwenyezi Mungu ndani ya Quran anaitaja waziwazi hawa
wanaadamu wote wanakarma wanaheshima, kama vilevile mwanamume anatakikana
aheshimiwe na vilevile mwanamke anatakikana aheshimiwe, kama vile mwanamume
anadaraja kubwa mbele za mwenyezi Mungu kwasababu ni kumbe ambacho kinaroho ya
Mungu, daraja hili vilevile analo mwanamke kwasababu nae ni kumbe cha mwenyezi
Mungu.
Tunapojaribu kuisoma Quran na kuiangalia Quran
iliyowazungumza wanawake na daraja iliyowapa, tutaona ya kwamba daraja hilo
halina tofauti na daraja la mwanaume, kwa mfano Quran imewataja wanawake ambao
ni wanawake watakatifu kama ilivyowataja wanaume, Quran imemtaja Maryam (a.s)
ambae ni mama yake Nabii Issa (a.s) yakwamba ni mwanamke mtakatifu.
Kama ambavyo imemtaja Fatma Zahraa (a.s) ambae leo
tunakumbuka mazazi yake katika aya tofauti, kama ambavyo imemtaja mlezi wa
Nabii Mussa (a.s) au Mke wa Firaun, Quran imemtaja mwanamke kwa kiwango hicho
na kwa daraja hilo na kwa heshima hiyo kama vile ambavyo imemtaja mwanaume kwa
heshima na kwa daraja tofauti alilokuwanalo.
Je, mwanamke
anamiliki? Katika Uislamu, mwanamke anayohaki ya kufanya kazi na kumuliki kama
anavyomiliki mwanamume? Mwenyezi Mungu anatangaza waziwazi ya kwamba kama
alivyokuwa mwanamume anayohaki ya kumiliki vilevile mwanamke anayohaki ya
kumiliki, mwanamke anayohaki ya kurithi? Ndio mwanamke hata baada ya kuolewa
vilevile anayohaki ya kurithi kama alivyokuwa mwanamume anayohaki ya kurithi.
Kwa ufupi yote tuliyoyasema ni katika kuzungumza daraja na
nafsi ya mwanamke katika dini ya Uislamu katika siku hii ambayo tunakumbuka
mazazi ya bint ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) bi Fatma bint Muhammad (a.s), katika
siku amabyo wanachuoni wameitangaza hii ni siku ya mwanamke duniani.
Kwamba mwanamke ni kiumbe kama kiumbe kingine cha kawaida,
jinsia zao ziko sawa, mapungufu kama yapo yapo kwa mwanaume na yapo kwa
mwanamke, wana haki sawa kama mwanamume anahaki na vilevile mwanamke anahaki
sawa.
Asanteni sana, Hongereni kwa siku hii nzito ya kuzaliwa ya
Mtume Muhammad (s.a.w.w) bi Fatma Zahra bint Muhammad (a.s) na siku ya Mwanamke
Duniani.
Imetolewa na
Maulana
Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Dhehebu
la Shia Ithnasheriya Tanzania. Tare : 26.02.2019, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar
es salaam.