Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa salamu za Krismas na Mwaka Mpya, leo Dar es salaam. |
TAARIFA KWA UMMA
SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA KWA WAKRISTO WOTE TANZANIA
NA DUNIA.
24/12/2017
Amani ya Mwenyezimungu iwe juu yenu nyote.Salam hizi za
Mkono wa Krismas kwa ndugu zetu Wakristo wa Tanzania na Wakristo wote Duniani wanaosheherekea
Mazazi (Kuzaliwa) kwa Nabii Issa (a.s) Mtume wa Mungu kwa ndugu
zetu wakristo ni Yesu Kristo.
Mkono huu wa
Kristmass, Mkono huu wa Eid ni Mkono uliobeba Umoja, ni mkono uliobeba
Mshikamano ni Mkono wa Eidi, ni mkono wa Krismaa uliobeba amani na Maelewano.
Lakini kubwa zaidi la kujiuliza na huenda wengi wakajiuliza swali hii kwamba
kwanini Viongozi wa Dini wa Kiislam katika siku hii ya kuzaliwa Yesu Kristo au
Nabii Issa (a.s) kwa Wiaslam, viongozi hawa wa Kiislam hususan Wafuasi wa
Madhehebu ya Ahlulbayt (a.s) au Mashia watoe Mkono wa Krismas,mkono wa
kheri,
mkono wa Baraka kwa
ndugu zao wakristo Watanzania na wa Dunia kwa ujumla ni kwasababu chache za
harakaharaka nitakazozieleza
Sababu ya kwanza tutambue
sisi Waislam na ndugu zetu Wakristo sote tunakusanywa na neon moja kwamba sisi
ni Waumini,
sote tunamuamini
Mungu mmoja ambae ndie aliyeumba Mbingu na ardhi na akawaumba wanadam wote hilo
la kwanza, Sote tunaamini kwamba kuna vitabu vya Mungu vilivyoshushwa hapa
duniani, tunaamini uwepo utumwa mitume wa Mungu na vilevile tunaamini siku ya
mwisho.
Kwahivyo kuyaamini
haya yanatukusanya sisi watanzania Waislam na Wakristo chini ya mwamvuli mmoja
wa imani, kwahivyo leo hii waislam tunapotoa mkono wa Krismas, mkono wa eid kwa
ndugu zetu wakristo ni kwasababu ni waumini wenzetu katika kumuamini Mungu
mmoja, katika kuamini siku ya mwisho na katika kuamini mitume waliotumwa na
kutuletea ujumbe hili la kwanza.
La pili kwanini
mkono wa Krimsaa kwa ndugu zetu Wakristo, ni kwasababu sisi wote
tunakusanya na anuani ya Utanzania, Waislam tulioko hapa ni Watanzania,
wakristo tulioko hapa ni Watanzania, kama sote ni watanzania ni wajibu wetu
sote kuilinda Tanzania yetu. Kama sisi Wislam na Wakristo ni Watanzania ni
wajibu wetu umoja na mshikamano wetu kama Watanzania, kama sisi sote ni
watanzania ni makosa makubwa kufungua mwanya wowote wa mvutano kati ya Waislam
na Wakristo hapa Tanzania, kwanini kwa sababu sote tunakusanywa ni
Utanzania.
Kwasababu sisi sote
ni watanzania ni lazima tuwe na sifa ya kuvumiliana, itikadi zetu, fikra zetu
na mitazamo yetu isitugawanye kwa kuwa sisi tunakusanywa na neon Utanzania,Na
Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa sisi waislam anasema “kupenda inchi yako ni katika
imani” kwahivyo leo hii sisi kama Viongozi na kama Waislam na kama Waislam Shia
Ithnasheriya tunapotoa Mkono wa Krisma, mkono wa Baraka na mkono wa Eid kwa
ndugu zetu Wakristo moja ni kuenzi huu Utanzania tuliokuwanao ambao ni kitu
muhimu na ni kitu kikubwa,Lingine ni kwanini tunatoa mkono wa Krismas,
ni kwasababu sisi
Waislam, Dini ya Uislam ni dini ya Mapenzi, Dini ya Uislam ni dini ya
kufahamiana, Dini ya Uislam ni dini ya amani, Dini ya Uislam ya kupendana,
anaeueleza Dini ya Uislam sio dini ya kupendana huyo hajauelewa Uislam.
Kwahivyo Uislam ni
dini ya Mapenzi, ni dini ya Maelewano ni dini ya Maelewano,Mtume Muhammad
(s.a.w.w) anatufunza siku zote anasema “ penda watu wapate kile ambacho
unachopenda ipate nafsi yako” kwahivyo Uislam ni dini ya upendo, uislam ni dini
ya Maelewanoni dini ya masikilizano leo hii tunapotoa mkono wa Baraka na mkono
wa kheri na fanaka katika Eid ya Krismass malengo makubwa ni kuwaonyesha ndugu
zetu wakristo kwamba Uislam ni dini inayompenda kila mtu, Uislani dini
iliyohimiza ujirani mwema na ujirani huu mwema hauwezi kudhibitika wala
kufanyika pasi na watu kupendana.
Kwahivyo mkono huu
wa Krismass ni mkono wa kuwaonyesha ndugu zetu Wakristo Wayanzania kwamba
Uislam ni dini ya mapenzi, kwamba uislam ni dini ya kuelewana, Sayyidina Ali (a.s)
kiongozi baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) anawausia watoto wake anawambia
“Hala hala nawahusieni majirani” Sayyidina Ali (a.s) alipokuwa anawahusia
watoto wake swala la Majirani, hajawaambia Majirani Waislam, hajawaambia
Majirani wachamungu la, kawaambia Majirani yaani majirani wote ima wachamungu,
Wakristo, Waislam na hata wasiokuwa na Dini.
Kwahivyo kitendo cha
leo cha sisi kutoa Mkono wa Krismass, mkono wa Kheri na Baraka kwa ajili ya
ndugu zetu watanzania wasiokuwa Wiaslam ni kutaka kuwaonyesha kuwa Uislam ni
dini ya mapenzi uislam ni dini ya maelewano.Nukta nyingine muhimu kwanini Mkono
wa Krismass,mkono wa Kheri na Baraka kwa ndugu zetu Wakristo kwa sababu
hakuna uadui kati ya Uislam na Ukristo, hakuna Uadui kati ya Waislam na
Wakristo,
Ukimsoma Mtume
Muhammad (s.a.w.w) na ukiisoma Qur’an yetu na ukisoma mwenendo wa watu
waliokuja baada ya mtume Muhammad (s.a.w.w) utapata yakwamba wanavyoueleza
Uislam, Uislam na Ukristo sio uadui kati yao bali ni Udugu na maelewano kati
yao.
Iangalie Qur’an
inavyowasemesha Wakristo inawaitaje, inawaita “Ahlul Kitabu” enyi watu
waliopewa Injili, enyi watu mliopewa Taurat, enyi watu mliopewa Zaburi hivi
ndivyo Qur’an inavyowasemesha Wakristo, kwahivyo Mkono huu wa Kheri na Baraka
ni kuonyesha ya kwamba hakuna Uadui hata kidogo kati ya Uislam na Ukristo, kati
ya Waislam na Wakristo.
Ukiisoma Qur’an,
Qur’an ina sura nzima inayoitwa suratul Mariam yaani sura ya Mariam, mariam
ambae kwa ndugu zetu Wakristo wanamwita “Bikira Maria” sisi kwetu Waislam
tunamwita “Mariam Mtakatifu” ni sura nzima inayobeba jina la Mariam, kwahivyo
lau Uislam ungelikuwa na Uadui na Ukristo kusinge kuwa na sura inayoitwa sura
ya Maria.
Vilevile ndani ya
Qur’an kuna sura ya Ruum yani sura ya Roma, Roma ni Wakristo ndani ya Qur’an,
na Waislam wanaisoma sura hiyo kila siku ya asubuhi na mchana
Mwisho nimalizie kwa
nukta yakwamba Kitendo cha sisi kutoa Mkono wa Kheri ya Krismass kwa ndugu zetu
Wakristo watanzania ni kuonyesha yakwamba Uislam ni dini ya Amani, Uislam ni
dini inayopenda watu wakae vizuri, Uislam ni dini inayopenda mahusiano mazuri
kati yao na ndugu zao Wakristo,
na kwamba Uislam
katika vitu inavyovipiga vita ni kitu kinachoitwa Ugaidi, Uislam na Ugaidi ni
vitu viwili tofauti, ni kuontesha ya kwamba Uislam hauna kitu ukatili kwa
wasiokuwa Waislam
Kitendo hiki cha
kutoa mkono wa Krismas kwa ndugu zetu Wakristo ni kuonyesha kwamba Uislam hauna
chinja chinja kwa Wakristo, Uislam hauna ukatili kwa Wakristo,
Uislam ni amani na
maelewano kwa Waislam na wasiokuwa Waislam.mwisho niwatakie ndugu zetu wakristo
Watanzania Eid njema, Krismass njema ya kusheherekea kuzaliwa Yesu Kristo au
Nabii Issa (a.s).
Na vilevile ni
itakie amani serikali yetu ya awamu ya tano ambayo imeweza kutufikisha hapa kwa
utulivu na kwa maelewano sisi Waislam Watanzania na Wakristo wa Tanzania, na
ninamuomba Mwenyezimungu Serikali hii awape hekima, awape busara ili waendelee
kutuongoza kwa salama na kwa amani na
vilevile
mwenyezimungu nchi hii azidi kuboresha maelewano kati yetu sisi Waislam na kati
ya ndugu zetu Wakristo, na yeyote ambae anania ya kuleta chokochoko ya kuvunja
amani hii, basi chokochoko yake isiweze kuingia katika nchi yetu ya Tanzania na
katika taifa hili, Mungu azidishe kulibakiza Taifa hili la Tanzania katika
Amani na kisiwa cha amani na mahala pa maelewano.Asanteni sana na Mungu
awabariki.
Imetolewa Na:
Kiongozi Mkuu wa Waislam
Shia Ithnasheriya Tanzania Maulana Sheikh Hemed
Jalala