Monday, April 13, 2015

Majambazi wamuua sista, wapora fedha



Majambazi wamemuua kwa risasi Sista wa Kanisa Katoliki Clencensia Kapuli (50) na kupora kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakijajulikana.
 
Wananchi wakiangalia sehemu ambayo majambazi walimpiga risasi Sista Clencensia Kapuli Ubungo, Riverside, Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga 

Pia, katika tukio hilo lililotokea jana saa nane mchana eneo la Riverside, Ubungo, Dar es Salaam, dereva aliyekuwa akimwendesha Sista Kapuli, Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.

Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mwenyeheri Anwarite, Makoka Jijini Dar es Salaam alikuwa mhasibu wa parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura aliyefika katika Kituo cha Polisi Urafiki kufuatilia tukio hilo alisema Sista Kapuli na sista mwenzake wakiwa katika gari aina ya Toyota Hilux, walikuwa wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha na walipita Riverside ndipo walipopatwa na mkasa huo.

“Bado hatujajua ni kiasi gani cha fedha kimechukuliwa kwa kuwa Sista Kapuli ndiye alikuwa mhasibu na ndiye aliyekwenda kuchukua fedha hizo, subirini tutakapokwenda benki kuuliza ni kiasi gani cha fedha alichukua na tutawajuza,” alisema Wambura.
Kamanda huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ukisubiri taratibu za mazishi.


Israel yakataa uchunguzi wa mauaji ya vita vya Gaza



Utawala wa Kizayuni wa Israel umepinga kufanyika uchunguzi kuhusu mauaji ya Wapalestina yaliyofanywa na jeshi la utawala huo katika vita vya siku 50 dhidi ya Ukanda wa Gaza. 


Danny Eifruni, mwendesha mashtaka mkuu wa jeshi la utawala wa Kizayuni ameliambia gazeti la Kizayuni la Haretz kuwa wanapinga kufunguliwa faili la uchunguzi kuhusu mauaji ya raia wa Palestina yaliyofanywa na wanajeshi wa Israel katika vita vya siku 50 vya mwaka uliopita dhidi ya Ukanda wa Gaza. 

Katika vita hivyo vya mwezi Julai mwaka 2014, zaidi ya Wapalestina 2,300 waliuliwa shahidi na zaidi ya wengine elfu 11 walijeruhiwa, wengi miongoni mwao wakiwa ni wanawake na watoto.

Wakati huohuo harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imesisitiza kuwa muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni utaendelea, lengo likiwa ni kuzikomboa ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. 

Sheikh Bassam as Saadi, mmoja wa maafisa waandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ametoa sisitizo hilo kufuatia kuuawa shahidi Wapalestina wawili katika shambulio la hapo jana la askari wa utawala haramu wa Israel huko Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. 

Amesema, taifa la Palestina halitoiacha amana ya Jihadi na muqawama bali litaendeleza harakati na njia ya mashahidi…/

Mufti asema unaweza 'kumla' mkeo Saudia



'Ni sawa kumla mkeo unapohisi njaa nchini Saudi Arabia lakini tu iwapo unahisi njaa kali'.
Mufti mkuu wa Saudia Abdul Azizi bin Abdullah

Mufti-kiongozi wa dini ya kiislamu aliye na uwezo wa kutoa uamuzi kuhusu maswala ya kidini-ametoa idhini ya ulaji wa mtu.

Kulingana na gazeti la Metro nchini Uingereza na mtandao wa Alalam nchini Saudia Abdul Azizi bin Abdullah alishtumiwa kufuatia tamko lake kulingana na mitandao mingi ya kiarabu.

Mtandao wa A Tayyar uliripoti:Mufti mmoja wa Saudi Arabia alitoa agizo ambalo linamruhusu mwanamume aliye katika ndoa kumla mkewe iwapo anahisi njaa kali.


Mufti huyo amesema kuwa hatua hiyo inaonyesha vile mwanamke anafaa kumheshimu mumewe.

Lakini mamlaka ya kidini yamekana kwamba kiongozi huyo alitoa matamshi kama hayo.


Chanzo http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2015/04/150411_grand_mufti?ocid=socialflow_facebook
Jamani huo sio mtazamo wa Kiislamu, kwani katika mafundisho ya Muhammad (s.a.w.w) pamoja na Maimamu 12 (a.s) hawajafundisha hivyo. 

Avigdor Lieberman ataka Wapalestina wote wauawe



Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel ametaka Wapalestina wote wauawe. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa IsraelAvigdor Lieberman

Shirika la habari la Palestina limemnukuu Avigdor Lieberman akisema hayo leo na kuongeza kuwa, hatarejea kwenye Baraza la Mawaziri la serikali ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, hadi pale Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS itakapofutwa kikamilifu na wanachama wake wote kuuawa. 

Lieberman ambaye ni mkuu wa chama cha Yisrail Beiteuni pia amemlaumu Benjamin Netanyahu kwa kukwepa mazungumzo ya muungano unaounda serikali ya utawala wa Kizayuni katika kuunda Baraza la Mawaziri. 

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa bunge la utawala wa Kizayuni "Kneset" wa tarehe 17 mwezi uliopita wa Machi, chama cha Likud kilipata viti 30, muungano unaojulikana kwa jina la "Umoja wa Kizayuni" ulipata viti 24 na muungano wa vyama vya Waarabu ukapata viti 13 kati ya viti 120 vya bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Israel, Baraza la Mawaziri linaundwa na chama kikuu lakini kiongozi wa kila chama atakayeweza kuunda muungano wenye viti vingi zaidi bungeni, hupewa yeye jukumu la kuunda serikali na Baraza la Mawaziri.
Chanzo http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/48042-avigdor-lieberman-ataka-wapalestina-wote-wauawe