Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa
Israel ametaka Wapalestina wote wauawe.
Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa IsraelAvigdor Lieberman |
Shirika la habari la Palestina limemnukuu Avigdor
Lieberman akisema hayo leo na kuongeza kuwa, hatarejea kwenye Baraza la
Mawaziri la serikali ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, hadi pale
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS itakapofutwa kikamilifu na
wanachama wake wote kuuawa.
Lieberman ambaye ni mkuu wa chama cha Yisrail
Beiteuni pia amemlaumu Benjamin Netanyahu kwa kukwepa mazungumzo ya muungano
unaounda serikali ya utawala wa Kizayuni katika kuunda Baraza la Mawaziri.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa bunge la
utawala wa Kizayuni "Kneset" wa tarehe 17 mwezi uliopita wa Machi,
chama cha Likud kilipata viti 30, muungano unaojulikana kwa jina la "Umoja
wa Kizayuni" ulipata viti 24 na muungano wa vyama vya Waarabu ukapata viti
13 kati ya viti 120 vya bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Israel, Baraza
la Mawaziri linaundwa na chama kikuu lakini kiongozi wa kila chama atakayeweza
kuunda muungano wenye viti vingi zaidi bungeni, hupewa yeye jukumu la kuunda
serikali na Baraza la Mawaziri.
Chanzo
http://kiswahili.irib.ir/habari/palestina/item/48042-avigdor-lieberman-ataka-wapalestina-wote-wauawe
No comments:
Post a Comment