Friday, August 7, 2015

Sheikh Mkuu wa al Azhar: kuwakufurisha Waislamu wa madhehebu ya Shia ni kitendo kisichokubalika

Sheikh Mkuu wa al Azhar nchini Misri amesema, kuwakufurisha Waislamu wa madhehebu ya Shia kunakofanyika kupitia kanali za televisheni za satalaiti ni kitendo kisichokubalika na jambo hilo haliwezi kuhalalishwa au kutetewa kwa kutumia kitabu kitakatifu cha Qur’ani, Suna na mafundisho ya dini.
Sheikh Ahmad al Tayyib amesema Waislamu wa madhehebu ya Suni wanaswali nyuma ya maimamu wa madhehebu ya Shia na kuongeza kuwa: Baina ya Shia na Suni hakuna hitilafu kubwa zinazoufanya upande mmoja uukufurishe na kuutoa katika dini upande mwingine na kwamba kinachoshuhidiwa kwa sasa na kutumiwa vibaya na kwa malengo ya kisiasa baadhi ya hitilafu za kimitazamo. 
Sheikh al Tayyib amesema wadhifa mkuu wa al Azhar ya Misri ni kufanya jitihada za kuunganisha Umma wa Kiislamu licha ya hitilafu za kimitazamo zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu. Sheikh Mkuu wa al Azhar amesema yuko tayari kusafiri na kwenda eneo lolote lile duniani kwa ajili ya kuimarisha umoja wa Waislamu.
Kwa kutilia maanani hali ya sasa ya nchi za Waislamu, inaonekana kuwa umoja wa Waislamu ndiyo wenzo muhimu zaidi ya kuwawezesha kuvuka salama fitina na njama za ubeberu na maadui wa dini hiyo ya Mwenyezi Mungu. Wakitumia mbinu mbalimbali, maadui hao wa Uislamu wamelifanya suala la kuanzisha vita na mapigano kati ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni kuwa ndiyo ajenda yao kuu kama njia ya kugawa na kuzusha hitilafu katika Umma. Nyenzo zinazotumiwa na maadui hao kwa ajili ya kupenya baina ya Waislamu ni kutumia wasaliti waliopotoka kutoka madhehebu mbalimbali za Waislamu na kisha kuhubiri tafsiri zisizo sahihi za kisiasa.
Kufasiri na kuhubiri Uislamu wa Kimarekani ni njama ambayo lengo lake ni kuzusha mpasuko na hitilafu katika safu za Waislamu na kuzuia ulimwengu wa Kiislamu kuwa nguvu kubwa katika siasa za kimataifa. Maadui wa Umma wa Kiislamu wanadhamini maslahi yao haramu kwa kuzusha na kukuza hitilafu ndogondogo baina ya Shia na Suni. Kwa njia hiyo maadui wa Umma wanawashughulisha Waislamu na masuala yasiyokuwa na umuhimu na kuwaghafilisha na mauala ya asili ya muhimu sana hususan kadhia ya Quds tukufu. Maadui hao wanaupambanisha Uislamu halisi na sahihi unaosisitiza umoja na mshikamano na ule wa fikra mgando unaowakilisha ujahili na ukatili. Mfano wa uislamu mgando ni ule wa makundi ya kigaidi ya Daesh, al Qaida na Boko Haram ambayo yote yanaungwa mkono kwa njia moja au nyingine na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Kama anavyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, katika maktaba na mfumo wa kifikra wa Imam Khomeini, Uislamu wa mashekhe vibaraka wa watawala, Uislamu wa Daesh, Uislamu usijali na unaokaa kimya mbele ya jinai zinazofanywa na Marekani na Israel na kunyoosha mkono wa udugu na urafiki kwa madola ya kibeberu unatokana na chanzo kimoja na hauwezi kukubalika.
Kwa msingi huo Waislamu wanapaswa kuwa macho na wasiruhusu maadui kutumia vibaya hitilafu zao za kimaoni na kimitazamo.

Mbatia Asema Neno Suala la Pro Lipumba

Kufuatia uamuzi wa Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), watu mbalimbali wamekuwa na mtazamo tofauti huku wengi wakitaka kujua hatua hiyo imepokelewa vipi na viongozi wa Ukawa.
Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia ameelezea jinsi alivyopokea taarifa za hizo akiwa mwenyekiti mwenza wa Ukawa.
Akiongea katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, Mbatia amesema kuwa uamuzi huo ni wa kawaida kwa kuzingatia mfumo wa vyama vingi nchini na kwamba Profesa ametumia uhuru wake kwa mujibu wa sheria.
Hii ni sehemu ya kauli ya James Mbatia:
“Ibrahim Lipumba kujiuzulu nafasi ya uenyekiti katika wa Chama Cha Wananchi CUF ni jambo la kawaida, ni mambo ya kawaida kabisa! Kwa sababu  tangu mfumo mzima wa vyama vingi vya siasa ulipoanza hapa Tanzania mwaka 1992 na vikaanza kuruhusiwa kufanya kazi kisheria, kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, ni kwamba kila chama cha siasa ni chama shindani cha mwenzake.
“Profesa Lipumba amegombea urais mwaka 1995, 2000, 2005, ni kiongozi anaefahamika Tanzania hapa na katika siasa za vyama vingi na mchango wake mkubwa kwa taifa. Lakini hatua aliyofikia…amefikia hatua yake yeye binafsi ndani ya chama chake cha CUF. Lakini tujue kwamba kuna haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Kauli yake aliyoitoa leo ni kwamba ataendelea kuwa mwanachama wa CUF lakini amepumzika kwenye uongozi ili apatikane mwanachama mwingine aweze kukiongoza chama hicho.

“Hivi vyama vya siasa ni Taasisi, binadamu sisi tupo tunapita tu na muda wetu ukifika tunafariki, lakini Taasisi zinabaki. Mwalimu Nyerere ndiye muasisi wa TANU na CCM, mwalimu hayupo lakini CCM bado ipo. Kwa hiyo hii ni changamoto tu ya kisiasa inayotokea na hapa kwetu Tanzania mtu kutoka chama kimoja kwenda chama kingine imezoeleka”

Vyama APPT NA SAU Vyajiunga Ukawa

Wakati vyama vinne vinavyounda UKAWA, vimempitisha Edward Lowassa kugombea urais, vyama vingine vya SAU na APPT-Maendeleo vimetangaza kumuunga mkono mgombea huyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. 

Katibu Mkuu wa SAU, Ali Kaniki alisema chama hicho kimefikia uamuzi wa kuunga mkono umoja huo kutokana na nafasi kubwa iliyopo ya kushika dola. Kaniki alisema kwa sasa wana wanachama zaidi ya 500,000 nchi nzima, hivyo wanaamini kuwa na mchango katika harakati hizo. 

Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema chama hicho kinaamini mabadiliko kupitia kambi ya upinzani, hivyo wameamua kuunga mkono UKAWA. 

“Uchaguzi wa mwaka 2010, nilishika nafasi ya nne kwa kupata kura 96,000, lakini pia tuna madiwani watatu na wanachama wameongezeka kwa hivyo ninaamini mchango wetu utakuwa na nafasi kubwa UKAWA,” 
Mwenyekiti wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam, Joackim Mwakitinga alisema chama hicho kitakuwa tayari kuunga mkono mgombea mmoja kutoka CCM au UKAWA.
“Nafasi ya urais hatutasimamisha mgombea ila tutaunga mkono kati ya vyama hivyo wakati wa kampeni.”

CUF IMESEMA INAENDELEA KUBAKI UKAWA LICHA YA LIPUMBA KUJIUZULU

Baada ya Prof Ibrahimu Lipumba kujivua Uenyekiti wa CUF, Chama cha CUF kimesema kuwa kitaendelea kubaki UKAWA na kuulinda umoja huo. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma Ismail Jussa inasema hivi
"Leo tarehe 6 Agosti, 2015 Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacock, mjini Dar es Salaam na kutangaza kwamba amejizulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF).
Sisi kama Chama tumezipokea taarifa hizo na tunayaheshimu maamuzi yake. Ni haki yake ya kikatiba na haki ya kidemokrasia kufanya maamuzi anayoyaona yana maslahi kwake.
Bila shaka, Profesa Ibrahim Lipumba amekifanyia kazi kubwa Chama chetu katika miaka 16 ambayo alikuwa Mwenyekiti wetu, nafasi iliyomfanya awe kiongozi wetu mkuu. Kwa nafasi yake hiyo, pia ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa demokrasia katika nchi yetu. Tunaithamini kazi hiyo na tutaendelea kumheshimu kwa utumishi wake mkubwa kwa Chama chetu na nchi yetu. Tunamtakia kila la kheri katika mipango yake ya baadaye.
Chama Cha Wananchi (CUF) ni taasisi na kinaendeshwa kitaasisi. Ndiyo maana maamuzi yake yote yamekuwa yakifanywa kitaasisi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama. Kwa msingi huo, pamoja na ukweli kwamba kuondoka kwa Profesa Lipumba katika safu ya uongozi kutaacha pengo hasa katika kipindi hichi ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, tunawahakikishia wanachama na wapenzi wa CUF na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwamba Chama hichi hakitayumba

Ilani ya vyama vya ACT, ADC sasa hadharani, Ukawa na CCM Bado.

Wakati joto la Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu likiendelea kupanda, vyama viwili vya ACT-Wazalendo na ADC ndivyo vilivyokamilisha ilani zake na kutangaza kwa umma, huku viongozi wa vyama vingine wakitangaza kukamilisha kazi hiyo kabla ya kuanza kampeni.
Kitabu hicho cha ilani kwa kila chama, hubeba ahadi za kuwatumikia wananchi.
Vyama vya UDP, PPT-Maendeleo, Sau na CCK, jana walisema watakachokifanya kwa sasa ni kuboresha ilani zao kwa ajili ya uchaguzi.
Katibu Mkuu wa Sau, Ali Kaniki alisema wameshanza kufanya maboresho ya ilani yao kwa baadhi ya vipengele.
Mwenyekiti wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Joackim Mwakitinga alisema sehemu ya ajenda katika kikao cha ndani cha Agosti 15, mwaka huu ni kupiti ilani ya chama.
Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Nasoro Dovutwa alisema chama kinaendelea na maandalizi ya kupitia ilani ya chama hicho.
Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muhabi alisema ilani ni sehemu ya ajenda katika vikao vya kamati kuu ya chama hicho vitakavyoanza leo, ili kupitisha jina la mgombea urais, ubunge na udiwani.
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alijinadi akisema chama chao ndicho pekee kilichokamilisha kuandaa ilani.
Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema tangu mwaka 2005, chama hicho kimekuwa kikifanyia maboresho ya ilani yake.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila alisema hakutakuwa na mabadiliko makubwa katika ilani ya mwaka huu kutokana na ubora wake.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hivi karibuni, alibainisha kuwa ajenda ya kuandaa ilani itakasimishwa kutoka mkutano mkuu kwenda kamati kuu, ambayo itaanza vikao leo.
Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alisema jana kuwa baada ya kukamilika kwa ilani hiyo, itapitiwa na vyama vingine vinavyounda Ukawa ili kuijadili kabla ya kuitangaza rasmi kwa umma.
“Hiyo ndiyo itakuwa ilani ya Ukawa baada ya kupitiwa na chama na baadaye vyama vingine ndani ya Ukawa,” alisema Makene na kuongeza:.
“Kwa sababu tumeamua kuungana kwenye uchaguzi huu, basi kile tunachokusudia kufanya lazima tuwape na wenzetu wapitie kisha ndipo nasi tutangaze kwa umma.
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete hivi karibuni alisema halmashauri kuu ya chama hicho itabeba jukumu la kushughulikia maandalizi ya ilani.Chanzo.Mwananchi.

Vyama Pinzani Vyalia, Magufuli akaribishwa Ikulu

Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mhe. John P. Magufuli mara baada ya kuwasili katika hafla iliyoandaliwa.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mhe. Nape Nnauye, Mhe. Abdulrahman Kinana, Mhe. John P. Magufuli na Mhe. January Makamba wakijumuika kwa pamoja katika hafla hiyo.

Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Abdulrahman Kinana na Mhe. January Makamba wafika kwenye hafla maalum ya kumuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kumkaribisha Mhe. John P. Magufuli.
Mhe. John P. Magufuli akisalimiana na Mhe. Stephen Wassira baada ya kuwasili kwenye makao makuu madogo ya CCM Lumumba.

CUF Kilio, ADC Sherehe

Mgombea urais wa jamhuri ya muungangano wa Tanzania LUTALOSA YEMBA katikati akiwa na mgombea urais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar HAMAD RASHID kulia na kushoto ni mwenyekiti wa chama hicho ambaye sasa ni mgombnea mwenza wa urais bwana SAID MIRAJ wakifurahia mara baada ya mkutano mkuu kupitisha majina yao kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuuu ujao nchini Tanzania
 Mwenyekiti wa chama cha ADC ambaye sasa ni mgombea mwenza wa urais akizngumza na wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu leo
Naye mgombea wa Urais katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambaye hapo awali alikuwa ndani ya chama cha wananchi CUF mh HAMAD RASHID  amesema kuwa sasa Zanzibar  hakuna upinzani kwani chama Tawala CCM pamoja na CUF wameungana na kuunda serikali hivyo chama cha ADC kimekuja kutoa upinzani wa kweli na bhatimaye mwaka huu kufanikiwa kuchukua dola hiyo.


Aidha katika hatua nyingine mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama hicho chief liembe amemteua mwenyekiti wa chama hicho bwana SAID MIRAJ kuwa mgombea mwenza wa urais katika uchaguzi ujao
 Maadhimio hayo yamefikiwa leo jijini Dar es salaam katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo wanachama walipiga kura ya kuwa na imani na wagombea hao kuipeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 25 ya mwezi wa kumi mwaka huu.
Akizngumza na wanachama mara baada ya kuchaguliwa kunai nafasi hgiyo kubwa ya uongozi katika jamhuri ya muungano wa Tanzania chief liemba amesema kuwa ana imani kubwa sana kuwa atafanikiwa kushinda nafasi hiyo huku akitamba kuwa hadi sasa hajaona mgombea kutoka chama chochote nchini ambaye ana uwezo wa kupambana naye katika uchaguzi huo.

 Hamad Rashid Pamoja na Chifu Yemba mara baada ya kuchaguliwa kugombea nafasi za juu ya nchi katika uchaguzi mkuuu ujao
 Wakati vyama mbalimbali viukiendelea kujiweka sawa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nacho chama kipya katika uchaguzi huu chama cha ,,,,,,,,,ADC leo kmimetangaza wagombea wake wan a fasi ya urais wa Zanzibar pamoja na mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.


Baada ya mchakato mrefu wa kupitia na kusikiliza hoja za watia nia mbalimbali katika nafasi hiyo mchakato uliopitia katika vikao vyote vya chama hicho  hatimaye mkutano mkuu uliofanyika leo umepitisha jina la chief liemba kuwania nafasi ya urais wa jamhuri ya muun gano wa Tanzania huku jina la mlezi wa chama hicho HAMAD RASHID likipita bila kupingwa kuwania nafasi ya urais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia chama cha ADC.

Pro. Lipumba atoa Sababu za kunga'atuka leo hii

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba leo ametangaza kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.
Tamko hilo la Prof. Lipumba linahitimisha siku mbili za minong’ono na tetesi zilizogubika medani ya kisiasa nchini kuwa kiongozi huyo anaondoka katika chama hicho hali iliyolazimu wananchama, wapenzi na mashabiki wa kiongozi huyo kufurika makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam jana ili kujua hatma ya kiongozi wao huyo.
Akizungumzia sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.
Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.
Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.