Kiongozi wa
Waislamu Shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislam na Wataznaia kumuomba
na kumlilia Mwenyezi Mungu pamoja na kusoma Qur’an kipindi hiki cha Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani ili Mwenyezi Mungu atuondoshee janga hili la Ugonjwa wa
Corona katika Mitaa, Mikoa na Nchi yetu.
“Mwezi huu
wa Ramadhani kwa janga hili la Corona ndio muda pekee wa sisi Watanzania wa
kumuomba Mungu masaa 24 ili atuepushie na kutuweka mbali na janga hili la
Corona, na ndio mwezi pekee wa kukisoma Kitabu cha Qur’an malengo makubwa ni
balaa hili la Ugonjwa wa Corona atuepushe na alitoe katika mitaa, mikoa na nchi
yetu pia ndio nafasi pekee ya kuswali , kusujudu na kujaa Misikitini kwa ajili
ya kumlilia Mwenyezi Mungu ili atuondoshee balaa hili la corona” Sheikh Jalala
alisema.
Sheikh
Jalala alisema hayo jana wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika
Kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es
salaam na Kusema kuwa tunatakiwa kumshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na kuzingatia
tahadhari zinazotolewa na Wizara ya Afya, Wataalam na Mhe. Muft wa Tanaznia katika
jitihada ya kupambana na balaa na , janga na Ugonjwa huu wa Corona.
“Jambo kubwa
ni Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba bado katika ardhi yetu ya Tanzania Misikiti
yetu, Makanisa yetu na Nyumba zetu za Ibada hazija fungwa bado tunahudhuria
katika nyumba zetu za Ibada, mahudhurio yetu katika Nyumba zetu za Ibada ni
lazima kuchukua tahadhari ambazo zinatolewa na Wizara ya Afya na zinazotolewa
na Wataalam na iliyotolewa na Mhe. Mufti wa Tanzania” Alisema Sheikh Jalala.
Aidha Sheikh
Hemed Jalala alisema leo hii Dunia, sisi watanzania na Waislam wote Duniani
pamoja na sisi Wafuasi wa Ahalul bayt (Shia Ithnasheriya) tunaukaribisha mwezi
Mtukufu wa Ramadhani wa mwaka wa 1441, mwezi huu wa Ramadhani ambao
tunaukaribisha naomba tuukaribishe kwa haya maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya
Qur’an tukufu, Eenyi mlio amaini mmefaradhishiwa Kufunga kama ilivyo faradhishwa
funga kwa watu waliokuwa kabla yenu ili nyinyi muwe Wachamungu.
Hata hivyo
Sheikh Jalala alisema Jambo ambalo linatufanya tuseme ya kwamba tunaukaribisha
mwezi mtukufu wa Ramadhani wa mwaka huu kwa kuamini ya kwamba hakuna kwa kweli
wa kutuondoshea balaa hili la Corona na tatizo hili zito ila ni kumnyenyekea ni
kumlilia ni kumuomba Mwenyezi Mungu(swt), dua ni silaha ya muumini.