Saturday, April 25, 2020

Sheikh Jalala Ibada za Mwezi wa Ramadhani zitumike Kumuomba Mungu atuondoshee Ugonjwa huu wa Corona


Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala (kulia) akiwa pamoja na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania (TIC) Sheikh Abdallah Seif wakiukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Jana Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.
Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Sheikh Hemed Jalala amewataka Waislam na Wataznaia kumuomba na kumlilia Mwenyezi Mungu pamoja na kusoma Qur’an kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili Mwenyezi Mungu atuondoshee janga hili la Ugonjwa wa Corona katika Mitaa, Mikoa na Nchi yetu.

“Mwezi huu wa Ramadhani kwa janga hili la Corona ndio muda pekee wa sisi Watanzania wa kumuomba Mungu masaa 24 ili atuepushie na kutuweka mbali na janga hili la Corona, na ndio mwezi pekee wa kukisoma Kitabu cha Qur’an malengo makubwa ni balaa hili la Ugonjwa wa Corona atuepushe na alitoe katika mitaa, mikoa na nchi yetu pia ndio nafasi pekee ya kuswali , kusujudu na kujaa Misikitini kwa ajili ya kumlilia Mwenyezi Mungu ili atuondoshee balaa hili la corona” Sheikh Jalala alisema.

Sheikh Jalala alisema hayo jana wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika Kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam na Kusema kuwa tunatakiwa kumshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na kuzingatia tahadhari zinazotolewa na Wizara ya Afya, Wataalam na Mhe. Muft wa Tanaznia katika jitihada ya kupambana na balaa na , janga na Ugonjwa huu wa Corona.

“Jambo kubwa ni Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba bado katika ardhi yetu ya Tanzania Misikiti yetu, Makanisa yetu na Nyumba zetu za Ibada hazija fungwa bado tunahudhuria katika nyumba zetu za Ibada, mahudhurio yetu katika Nyumba zetu za Ibada ni lazima kuchukua tahadhari ambazo zinatolewa na Wizara ya Afya na zinazotolewa na Wataalam na iliyotolewa na Mhe. Mufti wa Tanzania” Alisema Sheikh Jalala.

Aidha Sheikh Hemed Jalala alisema leo hii Dunia, sisi watanzania na Waislam wote Duniani pamoja na sisi Wafuasi wa Ahalul bayt (Shia Ithnasheriya) tunaukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani wa mwaka wa 1441, mwezi huu wa Ramadhani ambao tunaukaribisha naomba tuukaribishe kwa haya maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’an tukufu, Eenyi mlio amaini mmefaradhishiwa Kufunga kama ilivyo faradhishwa funga kwa watu waliokuwa kabla yenu ili nyinyi muwe Wachamungu.

Hata hivyo Sheikh Jalala alisema Jambo ambalo linatufanya tuseme ya kwamba tunaukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani wa mwaka huu kwa kuamini ya kwamba hakuna kwa kweli wa kutuondoshea balaa hili la Corona na tatizo hili zito ila ni kumnyenyekea ni kumlilia ni kumuomba Mwenyezi Mungu(swt), dua ni silaha ya muumini.

No comments: