Monday, March 23, 2020

Sheikh Jalala amshukuru Raisi Magufuli na Muft wa Tanzania kwa Maelekezo dhidi ya Corona

Kiongozi wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Wandishi wa Habari katika Kusheherekea Siku ya Israa, Miiraj na Biidha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w), 22,03,2020 Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

Kwa kweli Tunapenda Kumshukuru Mh. Raisi John Pombe Magufuli kwa kusimama Kidete na Kupambana  kuhakikisha kwamba mpaka leo Ugonjwa huu bado unadhibitiwa kwa hali ya Juu na kwa kiasi Kikubwa, yote hayo ni kwa juhudi ya Mh. Raisin a Serikali yake.

Sisi kama Viongozi wa Dini ya Kiislamu na kama Wafuasi wa Dhehebu ya Ahalulbayt  (Shia Ithnasheriya) tunapenda Kumshukuru Mhe. Raisi na Serikali yake kwa Kazi nzuri kama ambavyo vile vile kwa mnasaba huu wa Israa na Miiraj na Kutumwa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

tunapenda Vile vile Kumshukuru Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi kwa Maelekezo yake makubwa na maelekezo yake mazito yanayoonyesha Uweledi , yanayoonyesha Utaifa  yanayoonyesha ni Mtu anaeitakia kheri Tanzania hii iwe ya amani, iwe Tanzania isiyokuwa na Balaa la Ugonjwa wa Corona wala aina zote za Maradhi, Tunapenda Kumshukuru kwa Maelekezo yake yote ambayo ameyatoa namna ya Kupambana na janga hili la Coron.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwa Baraka la tukio hili la Israa na Miiraj na Kupelekwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ninamuomba Mwenyezi Mungu balaa hili la Corona tatizo hili la Corona Mwenyezi Mungu alisambaratishe , Watanzania wabakie Salama kwa balaa hili la Corona, Mwenyezi Mungu iangalie Tanzania kwa Macho yako mawili ambayo hayalali, kama ulivyoiangalia inchi hii ukaifanya ni nchi ya amani na Utulivu Mungu iangalie Vilevile uiepushie na balaa hili la Corona. Israa, Miiraji na Biidha njema kwa Waislamu wote na kwa Watanzania wote. Asanteni Sana na Mungu awabariki.
Na: Maulana Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi wa Waislam Shia Ithnasheriya
Jumapili 22,03.2020, Dar es salaam.

No comments: