Sunday, May 3, 2015

Mawlana Hemed Jalala "Bingwa wa Amani ni Imam Ali (a.s) "

Mawlana Sheikh Hemed Jalala akitoa hotuba juu ya Sherehe za Kukumbuka Kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s), Msikitini Ghadir, Kigogo-Post, Dar es salaam.
sherehe hizo zimeandaliwa na Hawza Imam Jafar Swadiq (a.s)Amesema ni kwanini tukumbuke siku ya kuzaliwa kwake? Tunakumbuka siku ya kuzaliwa kwake kwanza kazaliwa siku ya Ijumaa, Siku ya Ijumaa kwa Waislam ni siku ya Amani.
ni siku ya Eid, ni siku ya Furaha. Pili Imam Ali alizaliwa tarehe 13 Rajabu, na tarehe 13 kwa kila mwezi ni siku ya furaha na ni siku ya Funga na ni siku nyeupe. Kazaliwa katika mwezi wa Rajab, na mwezi wa Rajab ni mojawapo katika miezi nne (4) mitakatifu na.                                                                          
.

Mawlana Sheikh Hemed Jalala akiongea na Vyombo vya Habari juu ya Kusherekea Kuzaliwa kwa Imam Ali (a.s), kwa hiyo siku ya kuzaliwa Imam Ali (a.s) tunaungana na dunia kuienzi amani, ambayo Imam Ali (a.s) ndio alieitilia Umuhimu.     
            
 Waislam, Wakristo,Masheikh, Wachungaji, Maskofu na Mapadri wanaamini kwamba utulivu wanaoupata katika sehemu zao za Ibada ni kwasababu ya kuenziwa Amani iliyopo.                    

Kiongozi yeyote wa kiroho awe Muslam au Mkristo atakapokuwa amani kwake sio muhimu huyo hatokuwa kiongozi wa Kidini.Tanzania iendelee kubakia kuwa kisiwa cha amani, maelewano kati ya Wakristo na Waslamu

No comments: