Afisa Mawasiliano Shirikisho
la Soka Tanzania Boniface Wambura amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB
zimeunda kikosi kazi (task force) kwa ajili ya kushughulikia matumizi ya tiketi
za elektroniki ambayo yalisimamishwa kutoka na changamoto mbalimbali zilizokuwa
zimejitokeza.
Amesema TFF na CRDB
zimefanya kikao cha pamoja jana (Machi 20 mwaka huu) kuhusu masuala ya tiketi
za elektroniki na kukubaliana kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya uboreshaji
matumizi ya mfumo huo.
Aidha amesema Kikosi
kazi hicho kitakuwa na wajumbe kutoka TFF na CRDB. Kwa upande wa TFF wajumbe
wake ni Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama, Evodius Mtawala, Ofisa Habari na
Mawasiliano, Boniface Wambura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu
Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga.
Hatahivyo amesema Rais
wa TFF, Jamal Malinzi ametoa shukrani za kipekee kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
benki ya CRDB, Dr. Charles Kimei ambaye alihudhuria binafsi kwenye kikao
akiongoza timu yake.
amesema ni imani ya
TFF kuwa mfumo wa tiketi za elektroniki ndiyo mkombozi wa ulinzi wa mapato
milangoni, na anaamini kwa pamoja TFF na CRDB zitafanikisha matumizi hayo ya
tiketi za elektroniki.