Khatbu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Amir Kasonso akitoa Khutba Jana katika Masjis Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam, akizungumzia Kuitukuza Qur'an. |
Khtabu wa Swala ya Ijumaa Sheikh Amir Kasonso amewataka
Waislamu kuipa kipaumbele kitabu Kitufu cha Qur’an katika kukitunza, kukienzi
na kufuata yaliyomo ndani ya Qur’an ili kuweza kupata mahitajio yote ya
mwanadamu katika Nyanja zote katika Maisha ya Kila Siku.
Sheikh Kasonso alisema hayo jana katika Khutba ya Swala ya Ijumaa , iliswaliwa Masjid Bilal Temeke, Jijini Dar es salaam, katika
Khutba yake akizungumzaia Utukufu na Ubora wa Quran tukufu.
“Sisi leo hii Waislamu tujiulize, Qur’an tunaitetemekea
katika unyenyekevu na ule kuitukuza Qur’an je tunacho?, na kitendo cha kuienzi
na kuyafuata yaliyomo ndani ya Qur’an tunayo? Huku ndiko kunyeyekea
kunakotakikana” Alisema Sheikh Kasonso.
Aidha Sheikh Kasonso alionyesha hali ya kusikitisha kwa kuwa
hali ya Waislamu wanaishi kinyume na mafundisho ya Kitabu chao kitukufu cha
Qur’an na kufanya kila wanaloweza bila ya kuwa na chembe ya Hofu ya kuiogopa
Qur’an.
“Leo hii tunatembea
Vingine na Qur’an yetu inatuambia vingine, Kila jambo katika Ulimwengu huu
tunalipeleka vile ambavyo tunaona sisi liko sawa, lakini si vile Qur’an
inataka, hii ni dalili yakwamba sisi sio wenyenyekevu, sisi hatuheshimu Qur’an,
hatuiogopi Qur’an” alisisitiza Sheikh Kasonso.
Hatahivyo, Sheikh Kasonso amewataka wazazi kuweza kuthamini
Kitabu kitufu cha Qur’an na kutokilinganisha na Vitabu vingine ambapo baadhi ya
wazazi wameonekana wako tayari kumnunulia Daftari mtoto wake kuliko kumnunulia
kitabu kitufu cha Qur’an.
“Leo hii mzazi hataile thamani ya kumnunulia mwanae Juzu la
Tsh.300/= ni mtihani Mkubwa, angalie Qur’an inavyodhalilika, lakini aende
akanunue daftari, atanunua hata Daftari 15 hadi 20, ikiwa Juzu Mzazi yuko
tayari mwanae aende hivyohivyo, hii ni dalili Qur’an haidhaminiwi” Sheikh
Kasonso alionyesha huzuni.