Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam, Sheikh Alhadi Mussa akifafanua jambo katika semina ya siku ya Quds iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, Katika Mkutano huo Sheikh Alhadi aliunga Mkono harakati za kuwafanya wazawa wa Palestina kuwa huru na wenye kuishi kwa amani. |
Sheikh Alhadi Mussa aliyasema hayo jana katika semina Maalum iliyowakutanisha wataalamu mbalimbali yenye lengo la kujadili hali halisi ya nchini Palestina, Mkutano uliofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Daresalaam.ambapo mgeni rasmi alikuwa Sheikh Alhad Mussa Salimu
“Suala la maisha ya wazawa wa Palestina ni suala la kila mmoja wetu duniani, tunapaswa kupaza sauti kuhakikisha hatua ya kuwanusuru wapalestina inafikiwa kwa haraka na hivyo kuwaondolea adha kubwa wanayoipata kila leo”Alisema Sheikh Alhadi Mussa.
No comments:
Post a Comment