Sunday, July 3, 2016

Sheikh Jalala aongoza Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislam, Kikristo na Wapenda Amani Siku ya Wapalestina.


Kiongozi Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akielezea tukio la siku ya Wapalestina mbele ya Vyombo vya habari katika Matembezi ya AMANI ya Siku ya Kimataifa ya Quds Dar es salaam.
 "ili dunia iwe na amani na mahala salama pa kuishi, ni lazima kuitetea na kuunga mkono mapambano dhidi ya unyanyasaji, dhulma na uonevu dhidi ya wapalestina kama alivyofanya Hayati Mwalimu Nyerere na Nelson Mandela kwa kukemea yanayotokea katika adhi ya palestina kwa kipindi kirefu kwani leo yapo Palestina ila kesho huenda yakaenea ulimwengu mzima."alisema Sheikh Jalala

 Sheikh Jalala amesema athari ambazo zinajitokeza Palestina zinatisha, sasa Wapalestina wamekuwa kama wakimbizi katika Taifa lao, jambo ambalo si haki kwani wanastahili kuachiwa maeneoa yao ili waweze kuishi kwa Amani kama Tanzania nan chi zingine Duniani zinavyofanya.

Matembezi ya Amani ya Quds yanafanyika kila Ijumaa ya wiki ya mwisho wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, lengo likiwa ni kuwaunga mkono Waarabu wa Palestina wanaodhulmiwa mali zao, ardhi yao na kubomolewa makazi yao. Mpaka sasa tayari jumba Zaidi ya Elfu 45 zimeshabomolewa toka mwaka 1967.

Hayo alisema Juzi katika Matembezi ya AMANI  ya Siku ya Kimataifa ya Wapalestina (Quds) ambapo matembezi hayo yalianzia Ilala Boma hadi Kiwanja cha Pipo Kigogo Post Dar es salaam, na Siku ya Quds huadhimoishwa kila siku ya Ijumaa ya Mwisho ndani ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.







No comments: