Sunday, May 20, 2018

"Tunazindua Ubalozi Tel Aviv wakati Wapalestina wanaomboleza miaka 70 ya Kuvamiwa:?" Abdallah Othman


Image may contain: 3 people, people smiling
Uzinduzi/ Ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Israel leo tarehe 08/05/2018. Shughuli hiyo imefanywa na Mhe Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustine Mahiga pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Masima. Ubalozi huo wa Tanzania ulitambuliwa rasmi mwezi Mei 2017.

KAMATI YA MSHIKAMANO WA TANZANIA NA PALESTINA

Tamko kwa Umma
Tunazindua ubalozi Tel Aviv wakati Wapalestina wanaomboleza miaka 70 ya Nakba
(Janga au Kuvamiwa)

HATIMAYE nchiye tuimefungua ubalozi wake huko Israel. Waziri wa mambo yanje na uhusiano wakimataifa Dk. Augustine Mahiga amezindua ubalozi huo mjini Tel Aviv na kuikaribisha Israel nayo ifungue ubalozi wake nchini Tanzania.  

Tunaambiwa yote haya yanatokana na sera yetu mpya ya Diplomasia ya Kiuchumi inayolenga mahusiano yenyemaslahi yakiuchumi na nchi yoyo teduniani. Hatuna pingamizi nahilo ila tunatahadharisha isitupeleke kuja kuregeza misimamo yetu madhubuti iliotupaheshima katika anga za kimataifa na misimamo ilioasisiwa na Baba wa Taifa,nayo nikupinga Ukandamizwaji,Uonevu na Ukoloni mambo leo.

Ndipo tunajiuliza, hivi enzi zile za utawala wa makaburu kule Afrika Kusini tuliwasusia na kuwalaani kwasababu hatukuhitaji misaada au kwasababu ya msimamo wetu dhidi ya ukoloni na ukandamizaji?

Ufunguzi wa ubalozi tunasikitika umekuja katikakipindi kibaya, mwezi ambao ndugu zetu Wapalestina wanaadhimisha miaka 70 ya NAKABA, au JANGA, wakati ambapo nchi yao ilivamiwa na Wayahudi na wao kufukuzwa na kufanywa wakimbizi.

Wapalestina mwezi huu wote wanaandamana kupinga uporaji wa ardhi yao na uonevu wanaofanyiwa na kuuliwa bila hatia yoyote.Hiki kilikuwa siokipindi MUWAFAKA cha kufungua Ubalozi wetu kwambwembe zilezilokuwako. Huko nikuwatia unyonge nahuzuni ndugu zetu hao Wapalestina.
Kiongozi wa Wapalestina Yasser Arafat

Safari ya kwanza ya Kiongozi wa Wapalestina Yasser Arafat hapa Tanzania na alipokutana na Kamati ya Mshikamano ya Tanzania na Palestina aliwambia maneno haya, na nanukuu:

“Tulipokuwa katika mapambano yakuzuwia mauwaji yasio na hatia yanayofanywa na Askari wa ISRAEL kwa wakimbizi wa Kipalestina waliopo katika makambi ya SABRA na SHATILA tulipata faraja kubwa kusikia ndugu zetu wa Tanzania wanaandama na kulaani kwanguvu zote mauwaji hayo wakati Ulimwengu umekaa kimya na hata ndugu zetu wa nchi za Kiaarabu wako kimya. (Tanzania) ilikuwa ninchi ya kwanza ulimwengu kufanya hivyo kwakweli tulifarijika.”

Je leo hii katika kipindi hiki tunafungua ubalozi kwambwembe watajisikiaje ?
Hii ni Israel ambayo imewatia gerezani Wapalestina zaidi ya 6,000, wakiwemo watoto 304 na wanawake 63. Hawa ni wafungwa wa kisiasa ambao wamefungwa chini ya sharia yakijeshi. Idadi yao inazidi kuongezeka kila siku.

Je sisi Watanzania tuna msimamo gani? Au nisuala la “maslahi ya kiuchumi” tu?
Wapalestina zaidi ya 51 waliuwawa na Askari wa Israel katika nchi yao mnamo 14 Mei 2018, Gaza

Watanzania tunaungana na Wapalestina katika siku hii ya maadhimisho ya NAKABA,kwa sababu mwaka 1948 majeshi ya Kizayuni yaliteketeza vijiji na miji ya Wapalestina zaidi ya 530,na kuwafukuza Wapalestina 750,000 kutoka nchi yao ya  Palestina kwa mtutu wa bunduki 

Wapalestina takriban 750,000 wakaporwa asilimia 78 ya ardhi yao na kugeuzwa wakimbizi. Wapalestina zaidi ya 15,000 waliuliwa.
Hili ni janga kubwa katika historia na maisha ya Wapalestina. Kwa Kiarabu wanatumia neno “Nakba”. 
[​IMG]
Kwa mujibu wa takwimu za utawala wa Kizayuni wa Israel kuna watoto 437 Wapalestina wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala huo.

Hivi ndivyo nchi ya Palestina ilivyofutwa katikar amani ya dunia na badala yake wakabuni nchi yaIsrael kwa ajili ya Wayahudi. Na hivi ndivyo wanavyosheherekea “uhuru” waokila mwaka. Je, tuna msimamo gani kuhusu Nakba?

Leo hii zaidi ya Wapalestina milioni saba wamelazimishwa kuwa wakimbizi wakiishi katika nchi mbalimbali duniani. Wengi wao wanaishi katika kambi za wakimbizi katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi, Ukanda wa Gaza, Lebanon, Jordan, Syria na kadhalika.
Wakimbizi hawa wanazuiwa na Israel kurudi makwao kwamjibu wa sharia ya kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa. Katika Gaza maelfu wamekuwa wakiandamana kwa muda wa miezi miwili sasa wakidai haki yao ya kurudi walikofukuzwa tangu 1948.

 Matokeo yake nikupigwa risasi za moto na wanajeshi wa Israel.
 Siku moja baada ya Tanzania  kuzindua ubalozi, Wapalestina  zaidi ya 50 wameuwawa wakiandamana dhidi ya hatua ya Marekani kufungua ubalozi Jerusalem. (wakiwemo watoto na wanahabari wawili). Zaidi ya 5,500 wamejeruhiwa. Sikumoja tu!
Hivyo, Nakba iliyo anza miaka 70 iloyopita (mwaka 1948) ingali inaendelea hadi leo. Kila siku Wapalestina wamekuwa wakikabiliana na risasi za moto, vifaru, ndege za kivita na makombora. 

Makazi yao na mashamba yao yamekuw ayakiteketezwa,  ardhi zao zinaporwa, wanakamatwa na kufungwa katika magereza chini ya sharia za kijeshi. Hivyo haku na Mahakama wala mashtaka bali huteswa na kudhalilishwa. Ni pamoja na watoto na wanawake   
Wazayuni wanadai bila aibu kuwa wanafanya yote haya eti “kujilinda”.

Leo hii tunapozindua ubalozi huko Tel Aviv nivizuri tukakumbuka majanga yanayowapata wenzetu Wapalestina wanaoendelea kukandamizwa. Tukumbuke msimamo aliokuwanao Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ambae mnamo 1984 (kabla ya kung’atuka) alisema:
Baba wa Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere

“Siku zote tumekuwa na msimamo usioyumba wa kuunga mkono haki ya Wapalastina ya kujitawala. Sisi Watanzania tulipokuwa tunadai uhuru wetu tulifanya hivyo tukiwa nchini mwetu. Wapalestina hali yao ni mbaya zaidi. Ni kwasababu wameporwa nchi yao na wamekuwa taifa lisilo na nchi. Ndio maana wanastahili kuungwa mkono siyo tu na Tanzania bali na Ulimwengu mzima. Dunia lazima iwasikilize kilio chao, iwaelewe na iwaunge mkono” 

Huu ndio msimamo wa Kamati yetu. Tunatumai ungali ni msimamo wa Nchi yetu ya Tanzania.
Kuheshimu utu wa mwanadamu duniani kote imekuwa daima ni tunu ya taifa letu tangu enzi za Mwalimu. Tuendelee kutunza tunu hii ili tusije tukasaliti msimamo wa taifa hili.

Abdullah M.Othman
Mwenyekiti
Kamati ya Mshikamano wa Tanzania na Palastina
Dar es Salam                                                                                    15 Mei 2018