Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala akigawa maji kwa baadhi ya wakazi wa kata ya kigogo Mbuyuni mara baada ya kuzindua programu ya kugawa maji na vipeperushi bure jijini Dar es salaam. |
Kiongozi Mkuu wa Waislamu Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed
Jalala, Mchungaji kanisa la Tanzania Outreach Ministries Banza Suleiman na Mwenyekiti wa Kata ya Kigogo Mbuyuni Bw. Hassan Nguogani wakikata utepe kuzindua programu ya kugawa maji na vipeperushi burejijini Dar es
salaam.
Habari Kamaili
Waislam wa dhehebu la
shia katika kuelekea siku ya Ashura Leo tarehe 10 ya muharram ambao ni sawa na
mwezi wa kwanza katika kalenda kiislam wamezindua program ya ugawaji maji na
vipeperushi bure iliyofanyika katika msikiti wa kigogo jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo msikitini hapo Sheikh Jalala amesema kuwa
zoezi hili la kugawa maji linaendana sambamba na kumuenzi Imam Hussein ambaye
ni mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume Mohamad ambaye alifariki kwa kuwatetea
wanadamu bila kuangalia itikadi zao za kidini, kikabila wala maumbile.
Sheikh
Jalala alisema imam hussein amekuwa ni alama kwa dunia kwa kukubali yeye kufa
ili watu wapate amani pamoja na kutendeana mema ikiwemo kupendana, kuhurumiana
kuheshimiana na alithubutu kuyafanya hayo wakati huo ambao mema yalipungua
katika dunia na hakukuwepo amani miongoni mwa wanadamu hao na matokeo yake
yalikuwa ni ugomvi na chuki ndani ya kizani hicho.
Alisema Imam Hussein
anatufundisha watanzania kuwa ni watu wenye huruma, upendo ushirikiano na amani
tuliyopewa kama nuru yetu Watanzania, ndiyo maana msikiti huu umeamua kuanzisha
program kama hizi ikiwemo kuwatembelea wagonjwa, kujitolea damu kwa hiari,
kwenda kuwapa moyo wafungwa pamoja na kuwaona na kuwapa misaada watoto yatima
ikiwa ni miongoni mwa njia za kumuenzi Imam huyo aliyejitoa kwa ajiri ya
wanadamu.
Kwa
upande wake Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Christian Outreach Ministries Mchungaji
Banza Suleiman alisema kitendo kilichofanywa na msikiti huo ni chema na
kinapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania anaependa maendeleo kwani maisha yetu
wanadamu yanategemea maji kwa kiasi kikubwa, hivyo ili kumuunga mkono Rais
Magufuli kufikia kuwa na uchumi mzuri wa viwanda ni lazima watu wawe na maji ya
kutosha ili waweze kufanya kazi ipasavyo.
alisema
mungu anambariki anaetoa hivyo kwa kujitolea huko mungu awabariki sana na hata
serikali itafurahi kwa kuona taasisi za kidini zipo kwa dhumuni la kuwajari
wananchi wake kama kitendo kilichofanywa na msikiti huo, pamoja na wananchi wa
maeneo hayo wataona ni jambo jema kutokana na maisha ya mwanadamu yanategemea
maji hivyo bila maji hakuna maisha.
Nae
Mwenyekiti wa Mtaa Kigogo Mbuyuni Bw. Hassan Nguogani alisema wanaishukuru taasisi
Shia kwa kuchangia maendeleo ya kata hiyo kwa kiasi kikubwa kwani imekuwa ikijitolea
mambo mengi kama matibabu bure kwa wagonjwa, kusaidia watoto yatima katika kata
hiyo kama madaftari na vifaa mbalimbali vya shule kwa wanafunzi na huduma
nyingine nyingi.
Aidha
Bw.Nguogani aliongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia
juhudi za kimaendeleo kama kupanda miti, kufanya usafi maeneo ya kata hiyo, kuchangia
ujenzi mbalimbali katika kata hiyo.
Alisema
taasisi hiyo imekuwa itatoa misaada na kusaidia kufanya majukumu mengi ambayo kimsingi
mengine utekelezwa na sreikali lakini taasisi hiyo wamekuwa wakijitolea hivyo
kuwanufaisha wakazi wa kigogo na nifahari sana kwa uwepo wa msikiti huo mahali
hapo.
|