Ripoti zinasema kuwa wafanya maandamano hao ambao jana
walikusanyika kwa wingi katika mji mkuu wa Mexico huku wakiwa wamebeba
bendera za nchi hiyo, wametangaza kupinga mipango ya Rais Donald Trump
wa Marekani ya kutaka kujenga ukuta wa mpakani na kuendelea kuwafukuza
wahajiri wa Mexico huko Marekani. 
Jumapili iliyopita pia maaandamano mengine kama hayo yalishuhudiwa
katika miji mbalimbali ya Mexico katika kupinga siasa za Marekani dhidi
ya nchi hiyo. Wafanya maandamano hao walisema kuwa wao wakiwa ni raia wa
Mexico wanapasa kuitolea mwito serikali itekeleze majukumu yake na
kuwalinda raia na mamlaka ya kitaifa mbele ya mashambulizi ya serikali
ya Marekani.
No comments:
Post a Comment