Kiongozi Mkuu wa Waislam dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema kuwa suala la kuwasaidia na kuwaunga mkono wajane ni jambo la dini zote, ni jambo la Waislam, ni jambo la Wakristo na ni jambo la Wasiokuwa na dini.
Amesema hayo leo katika futari ya pamoja na Wajane kwa kumbukumbu ya Kifo cha Mke wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Bibi Khadijah (r.a), Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam, iliyowakutanisha Wajane wa Dini zote na Madhehebu yote bila kujali Kabila.
Katika Futari hii ya Pamoja na Wajane Naibu Mwenyekiti wa chama cha wajane Tanania Mh. Mariam Dauson Aswile ni mgeni rasmi ambae amekuja kumuakilisha Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania,
Sheikh Jalala ametoa wito wa kila jamii kuweza kutambua idadi ya kila wajane waliopo sehemu husika kwanzia ngazi ya kijiji,Mtaa, Mkoa hadi Kitaifa ili iwe rahisi kuweza kuwasaidia wajane pindi wanapokuwa katika matatizo mbalimbali.
Aidha Sheikh Jalala ametoa wito kwa Viongozi wote wa dini Masheikh, Maaskofu, Maustadh, Mapadri jambo la kuwaangalia wajane iwe ni moja muhimu liliopo mbele yao.
Pia sheikh Jalala amesema Masheikh na Maimam, Mapadri na Maaskofu wasitosheke tu kuwahubiria waumini Misikitini na Makanisani bali kuwahudumia wajane ni ibada kama ibada zingine na moja ya majukumu yao katika jamii.