Kiongozi Mkuu wa Baqir Media Mr.Twalha Zuberi Ndiholeye akionyesha Huzuni katika Maadhimisho ya Kifo cha Imam Ali Ibn Muhammad al-Naq (a.s), Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam |
Jina : Ali Ibn Muhammad
Kuniya : Abul Hassan ath-Thalith
Lakabu yake : An-Naqi, al-Hadi
Baba yake : Muhammad Ibn Ali at-Taqi
Mama yake : Samana.
Kufa kwake : 3, Rajab, Mwaka 254
B.H, Samarra, Iraq.
Imam Ali bin Muhammad (a.s.) ni Imam
wa kumi kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume Muhammad Mustafa (s.a.w.w.). Kama
Maimam tisa wateule wa Mungu waliotangulia kutoka katika kizazi cha Mtukufu
Mtume (s.a.w.w.), Imam Ali bin Muhammad (a.s.) alikuwa ‘Masoom.’ (asiyefanya
dhambi wala kukosea).
Alikuwa ni mwakilishi wa Mtukufu
Mtume (s.a.w.w.) na wa Allah katika ulimwengu huu. Kwa wafuasi wake anajulikana
zaidi kwa majina yake ya lakabu (majina ya sifa), Naqi (twahiru) na Hadi
(mwongozaji) kuliko jina lake halisi. Majina yake mengine ya sifa ni pamoja na
Nuseh (mshauri), Ameen (mwaminifu), Faqueeh (mwanasheria), Tayyib (mtakatifu)
and Murthadha (mwenye kuridhiwa).
Kama walivyokuwa Maimamu wengine
wateule wa Mungu kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Imam Naqi (a.s.)
alikuwa hodari na mjuzi wa akili na hekima ya kipekee, ambayo huakisi kutoka
kwenye mwenendo wake kwa kipindi chake kifupi cha maisha.
Kusema kweli, Imam (a.s.) mwenyewe
ananukuliwa akisema kwamba Maimam wote wateule wa Mungu (pamoja na yeye)
wamebarikiwa ilmu ya kipekee waliyojaaliwa kwao na Mwenyezi Mungu; ilmu hii iko
katika sehemu 73 ambazo kwazo sehemu 72 wamepewa Maimam 12 na Allah (s)
anamiliki sehemu
zote 73.
“Ulimwengu huu ni soko: baadhi
wanavuna faida, wengine
wanapata hasara.” Amesema Imam Ali
Naqi
“Yule ambaye ana hofu ya Allah, watu
humuogopa, na yule anaye
mtii Allah, watu humtii.” Amesema
Imam Ali Naqi
“Husda hutafuna matendo mema na
kuleta adhabu (kwa hasidi).” Amesema Imam Ali Naqi
“Kuwachukiza wazazi, hupunguza
riziki na kuleta udhalilishaji.” Amesema Imam Ali Naqi
“Hasira ni ufunguo wa shida, lakini
chuki ni mbaya zaidi kuliko
hasira.” Amesema Imam Ali Naqi
Kipindi cha uimamu wa Imam Ali Naqi
(a.s.) ilikuwa ni “njia panda”muhimu ya kihistoria; kipindi hiki kimekuwa ni
mwanzo wa kukoma kwa utawala wa Banu Abbas ambao ulianzishwa na Mansoor na
kuletwa kileleni na Mamoon, na hatimaye kukoma katika mwaka wa 656 A.H. kwa
kuuliwa Khalifa wa mwisho wa Banu Abbas.
Imam Ali Naqi (a.s.) aliishi maisha
mafupi ya miaka 42 tu, nusu ya maisha haya akiwa ameyamalizia gerezani kwa aina
moja au nyingine, na pia akiwa nchi ya ugenini. Licha ya vikwazo hivyi, Imam
(a.s.) alihudumu katika njia ya Allah kwa uzuri sana na akaunganisha maisha ya
watu wengi wa hali zote za maisha.
Kwa hiyo alipendwa na kuheshimia na
watu wakati alipokuwa hai nakukumbukwa na wengi baada ya kufariki kwake. Ili
kuielezea nukta hiitutaleta rejea kwa ufupi ya mtazamo kutoka kwa wanachuoni
mashuhuri wachache wa Sunni juu ya mwenendo na mafanikio ya Imam (a.s.).
Ninarudia kutoa Pole kwa Bwana Mtume
Muhammad (s.a.w.w), na kwa Imam Mahd (a.s) pamoja na Waislam wote kwa Kifo cha
Mjukuu wa Mtume ambae ni Khalifa na Imam Ali Ibn Muhammad al – Naqi (a.s).
Wapenzi wasomaji kwa
mara nyingine ninatoa mkono wa pole na Simanzi kubwa kwa mnasaba wa kuzaliwa Imam Baqir (a.s), Imam
wa Tano katika Maimam aliowataja Mtume Muhammad (s.a.w.w) kuwa Makhalifa baada
yake, wakwanza akiwa ni Imam Ali Ibn Abu Taalib (a.s), Wapili ni Imam Hassan
Ibn Ali (a.s), watatu ni Imam Hussein Ibn Ali (a.s), wa nne ni Imam Ali Ibn
Husein -Sajjad (a.s) na Wa tano ni Imam Muhammad Ibn Ali al Baqir (a.s).
Imetolewa
na
Twalha
Zuberi Ndiholeye
Kiongozi
Mkuu wa Baqir Media
Tarehe
10/04/2015, sawa na 3, Rajab 1437
E-mail. twalhaz@gmail.com