Saturday, March 7, 2015

Maulama wa Kisuni watangaza jihadi dhidi ya Daesh



Maulama wa Kisuni katika mji wa Mosul Iraq, wametangaza vita vya jihadi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh linaloungwa mkono na Marekani. 


Maulamaa na mamufti

Maulamaa na mamufti wa mji huo wametangaza hatua hiyo katika kongamano lililofanyika mjini Erbil, Kurdistan ambapo pamoja na mambo mengine wametangaza kuwa, kundi hilo lisilofuata mafundisho ya Kiislamu, linawatumia raia wa mji wa Mosul kama ngao na kwamba wananchi wanatakiwa kupambana na matakfiri hao. 


Wanavyuoni hao wamefafanua kuwa, ni wadhifa wa maulama wa kidini kuisafisha sura ya Uislamu baada ya kuchafuliwa na kundi hilo hasa kwa kuzingatia kuwa, baadhi ya maulama huko Mosul wanalazimika kutoa fatwa zinazoendana na matakwa ya kundi hilo wakiwa chini ya mashinikizo na vitisho. 

Katika upande mwingine jeshi la Iraq limekama chombo cha kijasusi cha kielektroniki cha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kilichokuwa kikitumiwa na kundi hilo la Daesh. 

Kwa mujibu wa jeshi hilo, chombo hicho kimenaswa katika operesheni za kuukomboa mji wa Tikrit, makao makuu ya mkoa wa Salahuddin ambao umekaribia kukombolewa kikamilifu kutoka kwa magaidi hao na kwamba kimenaswa katika uwanja wa ndege wa ad Daur, mashariki mwa mji huo.